________________________________________________________

________________________________________________________

KAMPUNI YA BURUNDI YARIDHIKA NA UFANISI NA HUDUMA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Septemba 27, 2017

Kampuni ya MINOLACS ya Burundi imeahidi kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya kuridhika na ufanisi wa hali ya juu wa kuhudumia shehena ya ngano Tani 12,000 za kampuni hiyo hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Munir Bashir ameyasema hayo katika barua yake ya shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko ambapo pamoja na mambo ameelezea jinsi Bandari ya Dar es Salaam ilivyo na ufanisi bora wa huduma.

“Tunashukuru sana menejimenti ya TPA na wafanyakazi kwa utendaji wenu mzuri na wa hali ya juu uliowezesha kuhudumia shehena yetu iliyoletwa na meli ya MV Loving,” imenukuu sehemu ya barua hiyo.

Akifafanua zaidi Mkurugenzi wa MINOLACS imeongeza kuwa, “…tunawashukuru sana na tunaaahidi kuongeza shehena kufikia Tani 16,000 za ngano tutazopitisha Bandari ya Dar es Salaam wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba mwaka huu.”

MINOLACS ni Kampuni binafsi inayojishughulisha na biashara ya nafaka, kwa ajili ya chakula yenye uwezo wa mauzo ya kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 6.8 kwa mwaka.

Tayari TPA imefungua huduma zake katika nchi ya Burundi, mji wa Bujumbura ili kusogeza huduma zake karibu na wateja. Pia ina ofisi zake mjini Lusaka- Zambia, Kampala, Uganda, Kigali-Rwanda na Lubumbashi – Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo.

 ________________________________________________________

________________________________________________________

RWANDAN CARGO AT DAR PORT ON THE INCREASE

Septemba, 2017:

The Dar es Salaam port has witnessed an increase in Rwandan cargo passing through the facility to at least 950,000 tonnes in the last year from 630,000 tonnes for the period of 2012/13.

According to Tanzania Ports Authority (TPA), the increased number equals to 9.9 per cent.

TPA Director General Eng.  Deusdedit Kakoko revealed this in Dar es Salaam yesterday, when he met with Rwanda ambassador in Tanzania Eugene Kayihura who visited the port.

The TPA boss said presently cargo from Rwanda and other neighboring countries was stored within the port premises to ease clearance and ensure security of the cargo.

The Director General stated that in its strategy to strengthen business relations with customers, the government through TPA has allocated space for storage of Rwanda cargo at the Kwala dry port, in Ruvu and called for Rwandan traders to use that dry port for their cargo and the Isaka dry port in Shinyanga in order to reduce travel time.  He said that TPA has already completed the construction of its liaison office in Rwanda for serving its customers from that country and was working on finalizing all procedures before official inauguration.

The Opening of the office will greatly help to strengthen our service to Rwandan customers who are using the Dar e salaam port,”Eng.  Kakoko said.  The Rwandan ambassador Kayihura thanked the government of Tanzania for providing them with space to store Rwanda cargo.

Ambassador Kayihura said the trade between the two countries had been steadily increasing in recent years after TPA had improved its services.

“Currently the Dar es Salaam port has been handling at least 90 per cent of all imported goods from Rwanda, thus putting a record of rapid increase of  Rwandan cargo handled at Dar es Salaam port, ambassador Kayihura said. 

The ambassador said his visit to the port was part of Rwanda’s efforts to strengthen trade relations between the two countries.

In its strategy to ensure that the authority is close to its customers, TPA recently took part at the International trade fair in Rwanda where, amongst other things, Officials met with the country’s traders who were satisfied with Dar es Salaam port services.

MZIGO WA RWANDA WAONGEZEKA BANDARINI

Septemba, 2017:

Shehena ya Rwanda kupitia bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 9.9 kwa mwaka kutoka tani 630,000 mwaka 2012/2013 mpaka tani 950,000 mwaka 2016/2017.

Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko alipokutana na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura aliyetembelea TPA leo.

Kakoko amesema kwamba kwa sasa shehena yote ya mizigo inayokwenda na kutoka Rwanda na nchi zingine za jirani inahudumiwa ndani ya bandari ili kurahisisha uondoshaji na usalama wa mizigo hiyo.

Mkurugenzi Mkuu amesema katika mkakati wake wa kuimarisha uhusiano zaidi na wateja, Serikali kupitia TPA imetenga eneo kwa ajili ya kuhifadhia mzigo wa Rwanda katika bandari Kavu ya Kwala, Ruvu na kuwataka wafanyabiashara wa nchini Rwanda kuitumia bandari Kavu ya Isaka kwa ajili ya mizigo yao ili kuwapunguzia safari ya kusafiri hadi Dar es Salaam.

TPA tayari imeshakamilisha ujenzi wa ofisi yake nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudumia wateja wake toka nchini humo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, ofisi hiyo ya TPA nchini Rwanda imekamilika na kinachosubiriwa ni ufunguzi baada ya kukamilisha taratibu zote ili ianze kazi rasmi.

“Ufunguzi wa ofisi hiyo utasaidia sana kuimarisha huduma kwa wateja wetu wa Rwanda ambao wanatumia Bandari ya Dar es Salaam,” amesema Kakoko.

Naye Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura ameishukuru TPA na Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia eneo la kuhifadhia mizigo iendayo Rwanda.

Balozi Kayihura amesema kwamba biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni mara baada ya TPA kuimarisha huduma zake.

“Kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikihudumia asimilia 90 ya mizigo yote inayoingia na kutoka Rwanda hivyo kuweka rekodi ya ukuaji wa haraka sana wa mizigo ya Rwanda inayohudumiwa nchini,” amesema Mhe. Balozi Kayihura.

Amesema kwamba ziara yake aliyoifanya bandarini ni sehemu ya juhudi za Rwanda kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania haswa kwa kupitia huduma bora zitolewazo na Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.

Katika mkakati wake wa kuhakikisha inakuwa karibu na wateja wake, TPA hivi karibuni ilishiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa nchini Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine ilikutana na wafanyabiashara wa nchi hiyo ambao walionesha kuridhishwa na huduma za bandari ya Dar es Salaam.

BALOZI WA RWANDA NCHINI TANZANIA, MHE. EUGENE KAYIHURA NA MKURUGENZI WA TPA MHANDISI DEUSDEDIT KAKOKO WAKATI ALIPOTEMBELEA MAKAO MAKUU YA TPA HIVI KARIBUNI.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

S.L.P. 9184

DAR ES SALAAM

SIMU: (022) 2117816

________________________________________________________

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

Mahakama Yaamuuru Mali Zilizokamatwa Kwenye Tukio la Wizi Eneo la Bahari Kuu Zitaifishwe

Septemba, 2017:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeagiza kuwa mali zote zilizokamatwa katika tukio la wizi wa mafuta katika jahazi MV JITAZAME lililokutwa katika eneo la Bahari Kuu, Kigamboni zitaifishwe.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, G.A. Mwambapa ameagiza kwamba mali hizo ambazo ni pamoja na mafuta ya dizeli lita 15,570 iliyokutwa kwenye mapipa 50 na madumu 107 ndani ya jahazi hilo, boti, injini na pampu mbili za maji zitaifishwe kwa manufaa ya Serikali.

Awali akisomewa mashitaka, Kassim Ally Mfaume (49), Mkazi wa Unguja, Zanzibar, ambaye alikuwa Nahodha wa Jahazi hilo, aliieleza Mahakama kuwa mafuta hayo yanayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni thelathini, aliyanunua pamoja na wenzake katika meli moja eneo la Bahari Kuu na kuyaleta Kigamboni ili kutafuta wanunuzi.

Mahakama ilimtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kukutwa na shehena hiyo ya mafuta isivyo halali kosa ambalo mshatakiwa alikiri na kuadhibiwa kifungo cha miezi 18 au kulipa fani ya Tsh 1,000,000/=. Mshatakiwa alilipa faini na kuachiwa huru.

Mbali na mafuta hayo, Jahazi hilo pia lilikutwa na pump mbili za maji aina ya ‘Hitachi’ na injini moja aina ya ‘Yamaha’ (HP 60).

Uchunguzi wa awali wa polisi ulibaini kwamba Jahazi hilo MV Jitazame lenye usajili wa Zanzibar (Z – 1006) linamilikiwa na Bw. Ujude Abasi ambaye ni mkazi wa Unguja, Zanzibar.

Tukio la kukamatwa kwa shehena hiyo lilitokea mapema mwezi Agosti, mwaka huu majira ya saa 12.00 asubuhi ambapo askari wa TPA baada ya kupokea taarifa za kuwepo kwa jahazi lenye shehena kubwa ya mafuta likitokea Bahari Kuu kwenda eneo la Ferry-Kigamboni, walilifuatilia na kulikamata likiwa na shehena hiyo.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, inatoa tahadhari kwa watu wote ambao wana tabia ya kuingia maeneo ya bandari kwa lengo la kuiba mali za wateja, kuacha mara moja kwani vifaa vya ulinzi na usalama vilivyopo bandarini hivi sasa ni vya kisasa ambavyo vina uwezo wa kubaini wezi katika maeneo yote ya bandari. Tunawasihi kuithamini na kuilinda rasilimali hii muhimu kwa nchi yetu ambayo inatumika si kwa nchi yet utu bali na majirani zetu wanaotegemea kupitisha mizigo yao katika bandari yetu.

 

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

S.L.P. 9184

DAR ES SALAAM

SIMU: (022) 2117816

________________________________________________________

TPA YATOA MSAADA WA MASHUKA 900 KWA HOSPITALI ZA WILAYA YA TEMEKE

Agosti 29, 2017:

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashuka 900 yenye thamani ya Sh. Milioni Kumi kwa Hospitali za Temeke, Mbagala Zakheim na Round zilizopo katika Wilaya ya Temeke.

 

Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva ikiwa ni sehemu kutambua na kuthamini dhamira na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ya kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wote na hasa wa hali ya chini.

 

“Menejimenti ya TPA, chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, inaunga mkono kwa dhati kabisa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu, TPA inayo Sera ya Misaada kwa Jamii ambayo imejikita katika kusaidia jamii kwenye nyanja za Afya, Elimu na Maendeleo ya Kijamii,” amesema Mhandisi Kakoko.

 

Mhandisi Kakoko ameongeza kuwa pamoja na kwamba TPA kazi yake kubwa ni kuhudumia shehena mbalimbali zinazopita kwenye bandari zote nchini, lakini pia ina wajibu wa kurudisha kile inachokipata kutokana na huduma zake kwa kuisaidia jamii inayoizunguka na ndio maana imeamua kutoa msaada huo kwa Wilaya hii ya Temeke ilipo Bandari ya Dar es Salaam ambayo kiutendaji ndiyo bandari kubwa kuliko bandari zote hapa nchini.

 

Hivi karibuni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alizindua rasmi kuanza kwa kazi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam na mara itakapokamilika mwaka 2022 itaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli zenye uwezo wa kubeba kontena 8,000 kutoka kontena 2,500 za sasa na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani na kuliongezea Taifa mapato.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wanne kushoto) akishukuru kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (watano kushoto).

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wapili kushoto) akishukuru kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng Deusdedit Kakoko (watatu kushoto).

________________________________________________________

KATIKA PICHA: ZIARA YA WABUNGE WA BUNGE LA MALAWI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Agosti, 2017:

________________________________________________________

WAZIRI AAGIZA TPA KUFUNGA MASHINE ZA KUPIMIA MAFUTA NDANI YA MIEZI MITATU

Agosti, 2017:

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani,  ametoa miezi mitatu kuanzia sasa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuhakikisha kuwa mkandarasi wa ujenzi wa mita za kupimia mafuta (flow meter), eneo la Kurasini Oil Jetty (KOJ), amepatikana na kukamilisha ujenzi wa mita hizo ifikapo Novemba 2018.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri huyo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza mradi huo kumalizika ndani ya mwaka mmoja na ujenzi wa mita hizo kuhusisha bandari za Tanga na Mtwara. 

"Hakikisheni mnaongea  lugha inayofanana kati yenu na mtengenezaji ili kuepuka ucheleweshaji wa mradi huu ambao una tija kwa Taifa, pia hakikisheni mnapeleka wataalam nje ya nchi ili kuwajengea uwezo na kuongozea ujuzi na maarifa katika kusaidia kutekeleza mradi huu", amesema Eng. Ngonyani.

Ameongeza kuwa suala la ‘Flow Meter’, ni la ushirikiano kati ya Mamlaka hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wadau wengine wa mafuta, hivyo kukamilika kwake kutasaidia na kurahisisha  ukusanyaji wa mapato yatakayosaidia kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, amefafanua kuwa TPA ikifaulu kuwajengea uwezo wataalamu wake wa ndani, itasaidia usimamizi mzuri wa  uingizaji na uhakiki wa viwango vya mafuta yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salam, Tanga na Mtwara.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Ngonyani ametembelea na kukagua mitambo ya ukaguzi wa mizigo inayoingia bandarini (Scanner) na kuwasisitiza  wafanyakazi wa kitengo hicho kuangalia suala la uingizwaji  wa mizigo inayopita bandarini hapo  kwa mapana zaidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, amemhakikishia Naibu Waziri Ngonyani kutatua changamoto za Mamlaka hiyo na kutekeleza agizo la ujenzi wa flow meter mara moja.

Ameongeza kuwa TPA imetoa taarifa kwa Taasisi na Idara zote za Umma ambazo zinaagiza mizigo nje ya nchi kufanya mawasiliano na Mamlaka hiyo mapema kwa mizigo ambayo ni tofauti na ile ya kawaida ili kuongeza udhibiti na usalama wa mizigo hiyo.

Naibu Waziri Ngonyani amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Makao Makuu ya TPA na Bandari ya Dar es salaam na kujionea maendeleo  na changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo.

________________________________________________________

TPA donated 625 Roofing Sheets and 130 School Desks to Kalinzi Health Centre and Bangwe Primary Schools in Kigoma Region.

August, 2017:

________________________________________________________

PRESIDENTS MUSEVENI AND MAGUFULI LAY FOUNDATION STONE FOR CRUDE OIL PIPELINE MEGA PROJECT

August, 2017:

Tanzania President Hon. Dr. John Pombe Joseph Magufuli and his Uganda counterpart Hon. Yoweri Kaguta Museveni Commissioned the Construction of the 1,445km-long East African Crude Oil Pipe Line from Hoima District in Uganda to the Tanzanian Port of Tanga in Chongoleani Area.

The heated crude oil pipe line, the longest of its kind in the world, will cost $3.5 billion and will be completed by 2020 making Uganda join the ranks of oil producing countries. The pipeline works will be undertaken by Total E&P, CNOOC and Tullow Oil together with the two governments of Uganda and Tanzania. The pipe line will on completion carry 216,000 barrels of crude oil for export daily.

President Magufuli thanked President Museveni and his government for trusting Tanzania and choosing the Tanga route for the project despite the other options available. “This pipeline could have gone to a shorter route of 900kms but Museveni has supported us. We had to make concessions for our Ugandan brothers like we have previously done to liberate them,” he said.

The function was attended by Tanzanian Vice President, Hon. Samia Suluhu, the Prime Minister, Hon. Kassim Majaliwa and the Tanzanian First Lady, Madam Janet Magufuli.

QUICK FACTS ABOUT EAST AFRICA CRUDE OIL PIPELINE:

-       At 1,445kms, it will be the longest electrically-heated oil pipeline in the world.

-       Uganda will host 296kms of the pipeline, while the remaining 1,149kms will be in Tanzania.

-       In Uganda, the pipeline will run through eight districts and 24 sub-counties. In Tanzania, it will go through eight regions and 24 districts.

-       It will be a buried pipeline, with 1.2 metres of it beneath the ground.

-       Its estimated cost is $3.55 billion while constriction should last three years.

-       It will have a daily flow rate of 216,000 barrels with six pumping stations and two pressure reduction stations.

 

________________________________________________________

_________________________________________________________

WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI BANDARI YA KIWIRA KYELA!

Jumamosi, Julai 29, 2017:

Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja.

Meli hizo zimejengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine na zitatumika katika bandari za Kyela mkoani Mbeya.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ya Kyela kuwa walinzi wa meli hizo ambazo zinatarajiwa kutatua changamoto ya usafirishaji wa mizigo katika ziwa Nyasa na kuzitunza kwa maslahi mapana ya Taifa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TPA, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu), Mhandisi Karim Mattaka amesema ujenzi wa meli hizo zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja umekamilika kwa ufanisi mkubwa.

Mbali na kukamilika kwa meli hizo, TPA pia imeipa zabuni Kampuni ya Songoro Marine ya kuunda meli ya abiria na mizigo ambayo itakamilika hivi karibuni.

Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. Watatu kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Kyela Bw. Ajuaye Msese.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipatiwa maelezo na Harbour Master wa TPA, Capt. Mwingamno.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitizama mojawapo kati ya vyumba vya kupumzikia Mabaharia wa Meli hizo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipatiwa maelezo ya chumba cha mitambo 'engine' ya uendeshaji wa Meli hizo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Kyela ndani ya mojawapo kati ya Meli alizozindua.

Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira Wilayani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Karim Mattaka na Mkuu w Bandari ya Kyela, Bw. Ajuaye Msese wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa TPA na Manahodha wakati wa uzinduzi huo.

Meli mbili zilizonunuliwa na TPA zikiwa kwenye gati la bandari Kiwira Wilayani Kyela kabla ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

________________________________________________________

Tanzania and Uganda Ministers Signed Ministerial MoU

July 13th, 2017:

Tanzania Minister for Works, Transport and Communications, Hon. Prof. Makame Mbarawa (MP) and Uganda Minister of State for Transport, Hon. Bagiire Aggrey (MP), have Signed an ‘MoU’ on the Joint Ministerial Cooperation and Improvement of Ports and Inland Waterways and Railway Transport Services!

Tanzania Minister for Works, Transport and Communications, Hon. Prof. Makame Mbarawa (MP) delivers his keynote speech to delegates during the event held in Dar es Salaam on July 13th, 2017.

Uganda Minister of State for Transport, Hon. Bagiire Aggrey speaks to delegates during the event.

Tanzania Minister for Works, Transport and Communications, Hon. Prof. Makame Mbarawa (right) and Uganda Minister of State for Transport, Hon. Bagiire Aggrey (left), have signed ‘MoU’ on the Joint Ministerial Cooperation and Improvement of Ports and Inland Waterways and Railway Transport Services.

MoU signed between Tanzania and Uganda on the Joint Ministerial Cooperation and Improvement of Ports and Inland Waterways and Railway Transport Services.

TPA Director General, Eng. Deusdedit Kakoko gives an explanation about various port development to the Uganda Minister of State for Transport, Hon. Bagiire Aggrey (2nd left).

________________________________________________________

TICTS Kuilipa TPA Dola Milioni 14 Kodi ya Pango Kutoka Dola Milioni 7

Julai 06, 2017:

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni Binafsi inayoendesha Kitengo cha Kontena ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, TICTS zimetia saini mkataba mpya wa ambapo TICTS watakuwa wakiilipa TPA kodi ya pango (rental fee) Dola Milioni Kumi na Nne (14) kwa mwaka kutoka Dola Milioni Saba (7) za awali.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Mb.) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la utiaji saini amesema, “mbali na TICTS kulipa dola milioni 14, kodi hiyo pia itakuwa ikipanda kila mwaka kwa asilimia 3.8, hii inamaanisha kwamba kwa mwaka huu wakilipa dola milioni 14 mwakani watalipa dola milioni 14.8 na itaendelea kupanda kwa kiwango hicho kila mwaka.”

Prof. Mbarawa amesema tangu mwaka 2016 TICTS walikuwa wakilipa malipo ya aina mbili ambapo walikuwa wakilipa kodi ya pango Dola Milioni Saba (7) na kodi nyingine inayolipwa kwa kontena (throughput charges).

“Haijawahi kutokea leo unapangisha nyumba yako kwa shilingi laki moja kesho unamwambia mpangaji akulipe shilingi laki 2 akubali kwa urahisi, kwa hiyo TICTS sasa wamekubali kulipa dola milioni 14 kwa mwaka kutoka dola milioni saba, na zamani ilikuwa ukishaweka bei wanaendelea kulipa hiyohiyo lakini sasa kila mwaka itapanda kwa asilimia tatu (3),” ameongeza Prof. Mbarawa.

Kuhusu kodi ya kontena (kasha) TICTS sasa watakuwa wakilipa dola 20 kwa kila kontena na itakuwa ikiongezeka kwa asilimia nne (4) kila mwaka. Serikali imeiagiza pia TICTS kuhakikisha kwamba biashara ya bandari inakuwa na biashara ya kuhudumia kontena inakuwa kwa asilimia 6.5.

Mbali na ongezeko la mapato hayo pia eneo la ICD ya Ubungo ambalo lilikikuwa likitumiwa na TICTS sasa limerudishwa TPA na litakuwa mali ya Mamlaka. Mkataba baina ya TPA na TICTS ulisainiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 kwa miaka 10 ambapo mwaka 2015 mkataba huo uliongezwa tena kwa miaka 15 na ulitakiwa kuisha mwaka 2025.

Kusainiwa kwa mkataba huu mpya ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Maguuli alilolitoa hivi karibuni wakati wa ziara yake bandarini. Katika ziara yake hiyo Mheshimiwa Rais aliiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuupitia upya mkataba wa TICTS na mnamo tarehe 6 mwezi 10, 2016 Waziri Mbarawa aliunda timu ambayo leo hii imekamilisha kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo.

_________________________________________________________

_________________________________________________________

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

(TPA)

TAARIFA KWA UMMA:

 

KUHUSU KUKAMATWA KWA MAJAHAZI YENYE BIDHAA ZINAZODHANIWA KUWA ZA WIZI

 

JUNI, 2017:

 

Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kushirikiana na Askari wa Kikosi cha Jeshi la Polisi waliopo Bandarini, hivi karibuni walifanikiwa kukamata jahazi lenye jina la JITAZAME likitokea eneo la nangani (Outer Anchorage) nje ya Bandari  likiwa limepakia shehena kubwa ya mafuta ya ‘diesel’ yenye lita za ujazo 15,570 zenye thamani inayokadiriwa kufikia Sh. 30.9 milioni likiwa linayapeleka mafuta hayo maeneo ya Kigamboni.

 

Mbali na mapipa hayo jahazi hilo pia lilikutwa na madumu matupu sabini (90) yenye uwezo wa kubeba lita kati ya 40 na 70 kila moja yanayodhaniwa kwamba yalikusudiwa kutumika katika kubebea mafuta zaidi.

 

Juhudi zilifanyika za kulivuta jahazi hilo ambalo lilikuwa limeelemewa na mzigo huo hadi maeneo ya ferry na uchunguzi juu ya mmiliki halali wa mzigo na jahazi hilo unaendelea huku Polisi ikiwa imemkamata na bado inamshikilia Nahodha wa Jahazi hilo kwa mahojiano zaidi ili kujua mmiliki halali wa mafuta hayo na waliyatoa wapi.

 

Wakati huohuo katika eneo la meli za abiria bandarini alfajri ya tarehe 5/6/2017 lililetwa jahazi liitwalo REHEMA kutoka eneo la Kunduchi likiwa na mifuko ya sukari 88 na khanga kutoka India beli tano. Askari Polisi Kikosi cha Majini na Kikosi Kazi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania walifanikiwa kulileta jahazi hilo wakiwa katika operesheni maalum.

 

Mamlaka inawatahadharisha watu wote kujiepusha na vitendo vya wizi wa mali za Wateja au Bandari na endapo mtu au kikundi chochote kile kitakachokamatwa kwa kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

 

“Bandari ni Lango la Biashara, Kitaifa na Kimataifa”

 

Imetolewa na:

 

Menejimenti

 

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

Namba za Bure: 0800 110032 na 0800 110047

Tovuti: www.ports.go.tz

________________________________________________

Mkataba Maboresho Bandari ya Dar es Salaam Wasainiwa!

  • Rais kuweka Jiwe la Msingi hivi karibuni
  • Ujenzi wa gati jipya maalumu la Magari
  • Lango la bandari kuboreshwa
  • Kina cha maji kuongezwa hadi mita 15.5
  • Bandari kuhudumia mzigo hadi tani Milioni 28
  • Rwanda, Burundi, DRC, Uganda na Zambia kunufaika na SGR
  • Bandari kunufaika na kondolewa kwa VAT kwenye ‘transit goods’

Juni 10, 2017:

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Ukandarasi ya kutoka nchini China inayofahamika kama China Harbour Engineering Company Limited (CHEC) kwa pamoja wamesaini mkataba wa kuanza rasmi kwa kazi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (MB.) ameshuhudia tukio la uwekaji saini wa mkataba huku akisema kwamba ni historia kwa nchi yetu na kutoa wito kwa mkandarasi kuifanya kazi hiyo kwa weledi kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo na kamba Serikali haitavumilia ubabaishaji.

“Leo tunaanza kuandika upya historia ya Bandari ya Dar es Salaam ambapo tutashuhudia kazi hii ikianza na ujenzi wa gati la kuteremshia magari, kazi ya kuongeza nguvu na kuchimba kina cha maji katika gati namba 1 mpaka 7 pamoja na kuweka vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakulia mizigo, pia tumemuomba mkandarasi apunguze muda wa ujenzi na kuteremsha bei na amekubali,” amesema Prof. Mbarawa.

Pamoja na hilo Waziri ameongeza kwa bandari kuwa na kina kirefu ni jambo moja na haitoshelezi ndio maana Serikali imeamua pia kujenga reli mpya ya kisasa ya SGR yenye uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na kuwezesha treni kutembea kwa mwendo wa kasi zaidi wa kilomita 120 kwa saa.

“Kupitia reli hiyo mpya ya kisasa tunayoijenga (SGR), tunaamini tunaweza kushindana na bandari nyingine, nitoe mfano mdogo tu katika nchi jirani yenye bandari wao wamejenga SGR ambayo kusafirisha mzigo mpaka Kigali Rwanda (takribani kilomita 1,600) inawachukua saa 23 kufika Rwanda wakati kutoka bandari ya Tanzania mpaka Kigali (takribani kilomita 1,400) itatuchukua saa 13 pekee kufika Rwanda, jambo hili litawafanya Wafanyabiashara wengi kuitumia Bandari ya Dar es Salaam zaidi kutokana na kuwa na muda mfupi zaidi wa kusafirisha mizigo,” amefafanua Prof. Mbarawa.

Kwa upande mwingine Prof. Mbarawa amesema, “Nataka nitoe angalizo mapema kwa mkandarasi kwamba Serikali hii ipo makini (serious) na tunatarajia kazi hii itakamilika kwa kiwango na kwa mujibu wa makubaliano na hatutataka kuona viwango tulivyokubaliana havitekelezwi hatuvumilia jambo hilo hata kidogo,” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amesema, “Hadi kufikia mwaka 2025, TPA itaweza kuongeza mzigo kutoka tani za sasa milioni 14 kwenda mpaka tani milioni 28 mwaka 2022 na kama tusingejenga kwa mwaka huo wa 2022 tungeweza kuwa na tani milioni 20 kwa hiyo hii nguvu ambayo Serikali imeingiza itatuongezea ziada ya tani milioni 8,” amefafanua Eng. Kakoko.

Mradi huu umegawanyika sehemu mbili ambapo sehemu ya pili itahusisha kuchimba lango la kuingilia meli ili kupata mita 15. Sehemu ya kwanza inatarajiwa kuhusisha ujenzi wa gati jipya la kupakua mzigo wa magari (ro-ro), uimarishaji na uongezaji wa kina cha maji gati 1-7.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB.) akizungumza na wadau.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA na Watendaji Wakuu wa CHEC wakisaini mkataba huo.

Watendaji Wakuu wa TPA na CHEC wakibadilishana Mkataba mara baada ya kuusaini.

________________________________________________________

Wanabandari watakiwa kutumia Ushirika kujijenga Kiuchumi

Juni, 2017:

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wametakiwa kutumia fursa zinazotokana na kujiwekea akiba katika ushirika wao wa “Bandarini Saccos Limited” ili kujijenga kiuchumi na kujihakikishia maisha ya furaha na familia zao sasa na baada ya kustaafu.

Nasaha hizo zimetolewa karibuni na Ofisa Mkuu Biashara na Masoko wa TPA, Bw. Absalum Bohela kwa niaba ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam ambapo pia amewapongeza Viongozi wa Ushirika kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika ushirika huo. Bohela amewahimiza Wanachama kuendelea kuweka akiba na kutumia fursa ya mikopo kwa busara ili iwaletee tija katika maisha na familia zao kwa ujumla.

Amewaasa Watendaji wa Ushirika huo kuheshimu taratibu za uendeshaji kwa kuzingatia pande tatu ambazo ni pamoja na Uongozi, Wanachama na Watendaji ili kujenga ushirika wenye umoja na nguvu badala ya kuwa na vyama vingi ambavyo havina tija. Kwa upande wao Wanachama wa Ushirika huo wamesema Ushirika huo ukitumika vizuri utawawezesha kuondokana na umasikini na kupunguza utegemezi kwa Mwajiri katika baadhi ya mahitaji.

Semina hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam kwa awamu tatu ikiwahusisha wanachama 1,500 ambapo Katibu Mkuu wa Shirikisho Vyama vya Ushirika Tanzania (SCCURT), Bw. Habib Mhezi na Ofisa Ushirika Mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Amas Chacha walitoa mada mbalimbali kuhusiana na umuhimu wa kujiunga katika Ushirika, maana ya Ushirika na msingi na malengo ya Ushirika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Ushirika huo, Bi. Stella Mutayabarwa amesema semina hiyo imezingatia agizo la sheria na kanuni za ushirika kwa lengo la kuwajengea Wanachama uwezo na ufahamu zaidi kuhusu Ushirika. “Bandarini Saccos Limited” imeanzishwa mwaka 1968 na umekuwa katika hatua mbalimbali kwa kipindi kinachokaribia miaka 50 na mpaka sasa ina Wanachama takribani 1,700 huku ikiwa na mtaji unaozunguka wa zaidi ya Shilingi Bilioni 12.

\"\"

Viongozi wa Ushirika wa Akiba na Mikopo wa Bandarini Saccos Limited wa TPA, wakimsikiliza Ofisa Mkuu Biashara na Masoko, Bw. Absalum Bohela (katikati) wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanachama, Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Makamu  Mwenyekiti, Mataro Kikoba na Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo, Peter Mwasongwe.

\"\"
Ofisa Mkuu Biashara na Masoko, Absalum Bohela (wa pili kushoto), akiwa na Viongozi wa Ushirika huo wakati wa ufunguzi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Ushirika huo, Bw. Mataro Kikoba, wa pili kulia ni Mwenyekiti, Bi. Stella Mutayabarwa na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo, Bw. Peter Mwasongwe.


\"\"

Baadhi ya Wanachama, Viongozi na Wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada warsha hiyo.

\"\"

Wanachama wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa warsha hiyo.

______________________________________________________________

Wafanyakazi TPA waadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Juni, 2017:

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani hivi karibuni ambayo imefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo jijini Dar es Salaam kwa kuzihusisha Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Ujenzi.

Katika picha ni matukio mbalimbali kuhusiana na maadhimisho hayo.

\"\"

Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamuriho akiongea jambo na Wafanyakazi (hawapo pichani) namna Tanzania ya viwanda itakavyofanikiwa iwapo kutakuwa na mazingira mazuri.

\"\"

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho akipanda mti wa kumbukumbu kama alama ya utunzaji wa mazingira mwaka 2017.

\"\"

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakishiriki zoezi la kusafisha mazingira ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

\"\"

Wanafunzi wa Shule ya Mpakani wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

\"\"

Mfanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Mwanafunzi wa Shule ya Mpakani wakishiriki upandaji wa miti.

\"\"

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakishiriki katika kupanda miti katika maadhimisho hayo.

\"\"

Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi na wageni wengine waliohudhuria tukio hilo.

________________________________________________________________

Bandari ya Tanga inashiriki Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwahako, jijini Tanga.Maonesho hayo ambayo yamefunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage yatafanyika kwa siku kumi kuanzia  tarehe 28 hadi 6 Juni, 2017.

Uongozi wa Bandari ya Tanga unawakaribisha Wadau wote kwenye banda lake ili wapate kufahamu mambo mbalimbali kuhusu Bandari hiyo ikiwa ni pamoja na kupata huduma mbalimbali.

Katika picha ni matukio mbalimbali kuhusiana na uzinduzi wa maonesho hayo.

_______________________________________________________________________

 
Tanzania: Dar es Salaam Port Turns Up Roses With Increased Output, TPA Chief Now Reveals

 

APRIL, 2017:

 

Improved efficiency at the Dar es Salaam port has enhanced the volume of cargo handling, with promise of an additional 120,000 tonnes of imports and export to an annual freight tonnage of 16 million.

 

The Director General of Tanzania Ports Authority (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko, maintained yesterday that the volume of cargo has continued to record an upward trend during the last quarter of last year and first quarter of this year.

 

“We recorded an impressive surge in traffic of cargo between October and December, last year and this was maintained during January to March, this year,” he explained.

 

To spice-it all up, the Chief Executive Officer (CEO) of Simba Logistics Limited, Mr Azim Dewji, assured the port management of export and imports totalling 10,000 tonnes each month, translating to about 120,000 per annum.

 

Mr Dewji, a prominent businessman dealing in transport and logistics, hailed the Fifth Phase Government under President John Magufuli, for sweeping reforms at the port which have considerably improved efficiency.

 

The businessman was speaking at the port during an occasion to receive a fleet of over 50 long-distance trucks loaded with heavy machinery destined for mining and processing of minerals in the Eastern parts of Democratic Republic of Congo (DRC).

 

“We have clients in DRC who will be importing machinery for mining and construction projects and at the same time will be transporting through the Dar es Salaam port copper and other export from DRC and Zambia.

 

“… we had issues of red-tape from government authorities at the port in the past … but this is no more and we managed to secure a permit from TANROADS to transport the wide load consignment in just three days; it would have taken us weeks then,” he observed.

 

Mr Dewji revealed that there was an aggressive smear campaign from ports in neighbouring region, who want to tap into opportunities available in other land-locked countries in the region.

 

At the same occasion, the Director of MM Integrated Mills Limited, Mr Ratiku Kamania, said they were planning to import 10,000 tonnes of steel for its factories in Tanzania, Zambia, Uganda and Malawi.

 

“Almost 3,000 tonnes of the steel will be used in Tanzania and the rest will be exported to our factories in neighbouring countries,” he explained.

 

The DG of TPA had earlier disclosed that there were people trying to bypass the Tanzanian port despite its efficiency and proximity to mineral fields in Eastern DRC.

 

Source: All Africa/TMEA

_______________________________________________________________________

‘Simba Logistics’ kuitumia Bandari ya Dar es Salaam pekee!

 

Aprili, 2017:

 

Kampuni kubwa inayojihusisha na usafirishaji mizigo nchi mbalimbali, Simba Logistic imeahidi kuitumia Bandari ya Dar es Salaam pekee na kuachana na bandari nyingine za nchi jirani mara baada ya kuridhishwa na ufanisi wa huduma zake.

 

Ahadi hiyo imetolewa na Mmiliki wa Kampuni hiyo ya Simba Logistics, Bw. Azim Dewji mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

 

“Tunawahakikishia Watanzania na Mheshimiwa Rais kwamba mzigo wa Eastern Congo yaani Bukavu, Boma na Kivu sisi tutahakikisha mzigo wote unapita Bandari ya Dar es Salaam,” amesema Dewji.

 

Ameongeza kwamba wao kama Watanzania hawawezi kuona nchi kama Tanzania ikiwa na Bandari yenye ufanisi na barabara nzuri ikikosa mzigo kwa kupitishwa katika bandari nyingine za nchi jirani hivyo watahakikisha mzigo wote unapita hapa nchini.

 

Mapema akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amemshukuru Azim Dewji kwa kupitisha mizigo ya wateja wake bandari ya Dar es Salaam.

 

“Ndugu yetu Azim Dewiji akiwa ametambua juhudi za Serikali ameona ni vizuri atusaide katika kupata mzigo mpya ambao umetoka katika nchi jirani, kuanzia sasa mpaka mwakani kwa kipindi hiki tunaweza tukapata mzigo mpya ambao umepitia katika juhudi za Deweji wa tani laki moja na ishirini elfu,” ameongeza Kakoko.

 

Akizungumzia mzigo ambao kampuni ya Simba Logistics umeupitisha bandari ya Dar es Salaam, Kakoko amesema kama sio juhudi za Dewji za kutambua maboresho ya bandari ya Dar es Salaam, huenda mzigo huo ungepita katika bandari ya nchi jirani ambako imekuwa ikipita katika kipindi cha nyuma.

 

Wakati huohuo, Kakoko amezitaka Mamlaka mbalimbali zinazofanya kazi kwa namna moja au nyingine katika usafirishaji wa mizigo hapa nchini kuongeza ufanisi wa majukumu yao ikiwa ni njia ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi kutumia Bandari ya Dar es Salaam.

 

Baadhi ya Mamlaka zinazohusika na kutoa huduma za usafirishaji wa mizigo kutoka Bandarini ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) yenyewe, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jeshi la Polisi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Wizara ya Ujenzi, Tume ya Mionzi Tanzania (TAEC), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa Vipimo (WMA).

 

\"\"

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kushoto) akiwaonesha Waandishi wa Habari sehemu ya mzigo uliopitishwa Bandari ya Dar es Salaam badala ya Bandari jirani na Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistics Bw. Azim Dewji (kulia). Simba Logistics imepitisha mzigo huo Bandarini hapo mara baada ya kuridhishwa na huduma nzuri inayotolewa na Bandari ya Dar es Salaam.

 

\"\"

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na uamuzi wa Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistics (katikati) Bw. Azim Dewji kuamua kuitumia Bandarini ya Dar es Salaam mara baada ya kuridhishwa na huduma nzuri inayotolewa na Bandari hiyo. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Freddy Liundi.

 _______________________________________________________________________

 

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

MIAKA 12 YA KUANZISHWA KWA TPA

15 Aprili, 2005 – 15 Aprili, 2017

SALAAM ZA PASAKA!!!

 

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), leo inapotimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake mnamo Aprili 15, 2005, inapenda kutumia fursa hii kuwatakia Watanzania Wote, Wadau na Wateja wa Bandari ndani na nje ya Nchi, Pasaka njema yenye amani, utulivu na upendo.

Mamlaka inapenda kuwajulisha Wadau wake wote kuwa, Katika kipindi hiki cha miaka 12 tangu kuanzishwa kwake, TPA imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa bidii kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Bandari Na. 17 ya mwaka 2004.

Aidha, TPA imeendelea kuongeza ufanisi katika huduma zake kwa wateja kwa kuboresha miundombinu ya bandari, mifumo ya TEHAMA, kuendeleza Rasilimali Watu, kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama na kuboresha huduma za kimasoko kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.

TPA inapenda kutumia fursa ya kuadhimisha miaka 12 ya tangu kuanzishwa kwake, kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi mahiri na imara wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Serikali imekuwa Mdau Namba 1 kwa kuweka msumkumo mkubwa kwenye kuboresha miundombinu na utendaji katika sekta ya bandari kwa lengo la kuhakikisha bandari za Tanzania zinatoa mchango uliokusudiwa katika kuchochea maendeleo na uchumi wa Nchi yetu na Nchi jirani.

TPA inapenda kuwaahidi Watanzania na Wateja wake wote kwamba, itashirikiana nao katika nyanja mbalimbali katika kuhakikisha inatoa huduma zenye ubora wa kiwango cha kimataifa na zenye gharama nafuu. Lengo la TPA ni kuchochea mafanikio ya wateja wake katika nyanja za Kibiashara, Kiuchumi na Kijamii na hivyo kuchochea maendeleo ya Kiuchumi kwa Nchi yetu na Nchi jirani zinazotumia bandari za Tanzania.

Bandari za Tanzania ni Lango kuu la Biashara Kitaifa na Kimataifa na Kichocheo kikubwa cha Uchumi wa Viwanda kwa Nchi yetu na Nchi jirani.

_______________________________________________________________________

Treni za Mwendo Kasi kuongeza Ufanisi Bandari ya Dar

 

Aprili, 2017:

 

Kukamilika ujenzi wa reli mpya kwa kiwango cha ‘Standard Gauge’ kutaongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na reli hiyo kuwa na uwezo wa kupitisha treni za mwedo kasi kilomita 160 kwa saa na mizigo tani milioni 17 kwa mwaka.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb.) mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo iliyofanyika Pugu jijini Dar es Salaam, Aprili 12, 2017.

 

“Serikali yako ya awamu ya tano imeamua kujenga reli mpya kwa kiwango cha standardgauge yenye uwezo wa kuhimili uzito wa tani 35 kwa ekseli, pia yenye uwezo wa kubeba tani milioni 17 kwa mwaka ikilinganishwa na ya sasa yenye uwezo wa kubeba tani milioni 5 kwa mwaka,” amesema Waziri Mbarawa.

 

Ameongeza kwamba matokeo chanya yatakayopatikana kutokana na ujio wa reli hii ya kisasa ni mengi moja wapo ikiwa ni faida kubwa itakayopatikana kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambapo Bandari hiyo itaboreka zaidi na mizigo itatoka kwa haraka na kuwafikia wateja kwa muda mfupi zaidi.

 

Tofauti na reli ya sasa, reli mpya itakayojengwa kwa kiwango cha ‘standard gauge’ itakuwa na uwezo wa kupitisha treni za umeme za kisasa za mwendo kasi wa kilomita 160 kwa saa zikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani milioni 17 kwa mwaka ukilinganishwa na treni za sasa zenye uwezo wa kubeba tani milioni 5 kwa mwaka.

 

Pamoja na hayo, Prof. Mbarawa ameongeza kwamba reli mpya itakapokamilika usafari wa kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma utachukuwa saa 2 na dakika 50 na kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza itachukua saa 7 na dakika 40, tofauti na sasa ambapo inachukua saa 36 kufika.

 

Kukamilika kwa reli hii kutaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache ndani ya bara la Afrika zitakazokuwa na treni za mwendo kasi lakini pia kipekee zinazokwenda umbali mrefu tofauti na nchi nyingine ndani ya Afrika.

 

Nchi nyingine za Afrika zenye treni za mwendo kasi ni pamoja na Moroko kilomita 220 kwa saa na Afrika Kusini kilomita 160.

_______________________________________________________________________

 

Mwanza gears up for Uganda cargo… dry port in the works

April, 2017:

The dry port is part of an undertaking which Head of State, Dr John Magufuli, made at a joint meeting with Ugandan President Yoweri Museveni during his two-day State Visit to Tanzania last February. Dr Magufuli and his Ugandan counterpart agreed to maximize business opportunities that would boost the economies of their two neighbouring countries.

In 2016, business between Tanzania and Uganda stood at 178.19bn/-; it now stands at 193.59bn/-, according to Dr Magufuli. The two leaders also agreed to establish a dry port in Mwanza for Ugandan business people only, as well as repairing MV Umoja so that it can ferry goods from Mwanza to Uganda, in order to reduce the cost of transporting cargo.

The move was welcomed by his Ugandan counterpart who said it was the second liberation offered by Tanzania to Uganda after the support it offered Uganda in liberating the country from the dictatorial leadership of Idd Amin Dada.

“I salute the government of Tanzania for the envisaged construction of the Standard Gauge Railway and modernizing the Mwanza port as the services will now be cheaper, faster, more efficient and modern,’’ said Mr Museveni.

At the weekend, the Mwanza Region Business Development Officer, Mr Yesaya Sikindene, said already the port experts and regional leaders including Mwanza Regional Commissioner (RC), Mr John Mongella had visited the site where the dry port will be constructed.

However, he said that the cost of the construction was yet to be established, although he remains optimistic that everything was on course. “Immediately after construction of the port, it will be easier for the ships to ferry cargo from Mwanza to Uganda in an efficient and effective manner,’’ said Mr Sikindene.

During Mr Museveni’s visit, Dr Magufuli called for the need to exploit business opportunities to the maximum, urging Ugandan businesspeople, “should come and invest in the country … and Tanzanian traders to equally explore investment opportunities that are available in Uganda.”

Apart from the dry port, Tanzania is currently implementing a project for the construction of a Standard Gauge Railway from Dar es Salaam to Mwanza, Isaka, Rwanda and Burundi.

In an interview with the ‘Daily News’ in Mwanza the Mwanza RC said the completion of the Standard Gauge railway would help to maximize business in his region as it will be easier to carry cargo at the fastest and more efficient manner.

Source: Daily News

_______________________________________________________________________

ETHIOPIAN SHIPPING LINE TO CALL THE PORT OF DAR ES SALAAM

The Prime Minister of the Federal Democratic Republic of Ethiopia Hailemariam Desalegn commended the Port of Dar es Salaam for higher efficiency and said that the Ethiopian Shipping Line will start to call the Port of Dar es Salaam in a near future.

“I am glad to learn that the Tanzania Ports Authority is working very hard to make the service competitive so that when we use it will benefit our people,\" the Ethiopian Prime Minister when he visited the Port of Dar es Salaam briefly before flying back to Ethiopia yesterday.

He underscored the importance of marine transportation for the two nations to attain economic transformation and quicker economic volumes.

“…through our largest African Ethiopian airline our aviation group is keen to use port in transporting mechanism using the port transporting cargo as well by airfreight,” he noted.

He said his Government will send a team of experts to team up with Tanzania counterparts and identify areas of cooperation in transportation sector.  

While welcoming the Prime Minister of Ethiopia, the Tanzanian Prime Minister, Hon. Kassim Majaliwa Kassim expressed Tanzania commitment to strengthen further bilateral relations existing between the two countries. 

Earlier, the TPA Director General Eng. Deusdedit Kakoko briefed the Ethiopian Premier on activities of the Port and expressed commitment that Tanzania Ports Authority is committed to serve Ethiopia further in its unstoppable development.

“We are ready with such capacities to receive Ethiopian ships and cargo through efficient, effective and safe cargo hub, “Eng. Kakoko noted.

Eng. Kakoko said Ethiopian cargo will be handled safely through a fast-tracked and properly networked logistics of a surface and air intermodal transport system.

As such, he reiterated that TPA is prepared to Team-up with Ethiopian counterparts to make the dream of two countries a reality based on the fact that the political will has been created.

On his part the Minister for Works, Transport and Communications Prof. Makame Mbarawa commended the Federal Republic of Ethiopia for achievements made so far in terms of unprecedented industrial growth.

Prof. Mbarawa said the Government of Tanzania enjoys cordial diplomatic relations with the Ethiopian, urging that such relations be extended wider trade and economic relations.

He said already the Government of Tanzania has exchanged experiences on best practice from the Federal Democratic Republic of Ethiopia. In areas of economic policies, investments energy, transport, sports sectors and housing schemes among other key areas.

“We are particularly impressed by the fact that Ethiopia has made a notable industrial growth- the mission we share with our Fifth Phase Government under His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania,” he said.

 

Shirika la Meli la Ethiopia kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn amesema Shirika la Meli la Ethiopia (Ethiopian Shipping Line) lipo tayari kuanza kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kutoa huduma nzuri.

“Shirika letu la Meli ambalo ni la kihistoria na lililobaki pekee katika ukanda wa Afrika likiwa linamilikiwa na Serikali ya Ethiopia sasa lipo tayari kufanya kazi na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania,” amebainisha Mhe. Desalegn.

Ameongeza kuwa mbali na shirika hilo la meli kuwa tayari kuanza kuleta meli zake Bandari ya Dar es Salaam pia Shirika Kongwe la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airline) lenye mafanikio makubwa nalo litaanza kusafirisha mizigo inayopitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine Mhe. Desalegn amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Menejimenti ya TPA katika kuboresha huduma zake ambapo amesema jitihada hizo sio tu zitanufaisha Serikali zote mbili bali pia ustawi wa maisha ya watu wa Tanzania na Ethiopia nao utaimarika.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim amemshukuru Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa kuja nchini ambapo amemuahidi kwamba mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili yatadumishwa kwa maslahi mapana ya mataifa yote.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Makame Mbarawa amesema TPA itaendelea na mipango iliyopo ya kuhakikisha inaboresha Bandari zake ili ziweze kuhudumia vyema wateja wote kwa wakati.

“Tutaendelea kuboresha huduma zetu za Bandari na za sekta ya uchukuzi kwa ujumla ili tuweze kufikia malengo yenu na wateja wetu ya kuhakikisha kwamba tunawahudumia vizuri na kwa ufanisi,” amesema Mhe. Mbarawa.

Mapema akitoa taarifa ya utendaji wa Mamlaka, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimweleza Waziri Mkuu wa Ethiopia kwamba kwa sasa TPA inaendelea na mpango wake wa kujenga uwezo wa kuhudumia wateja wake kwa kuzingatia kwamba sekta ya uchukuzi inakuwa kwa kasi.

“Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi nchini na Duniani kwa ujumla, TPA inaimarisha uwezo wake wa kuhudumia mizigo na meli kubwa ili kujenga uwezo kabla ya mahitaji makubwa kujitokeza”, amesisitiza Mhandisi Kakoko.

\"\"

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim akisalimiana na Wakurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia.

\"\"

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kufika bandari ya Dar es Salaam.

\"\"

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko mara baada ya kufika bandari ya Dar es Salaam..

\"\"

Mhandisi Deusdedit Kakoko akisoma hotuba yake wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia bandari ya Dar es Salaam.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisoma hotuba yake wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Bandari ya Dar es Salaam.

\"\"

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn akizungumza na wageni wakati wa ziara yake Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

\"\"

\"\"

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Wakuu wa Taasisi kutoka Tanzania na Ethiopia.

\"\"

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim wakiwa katika picha na Wakurugenzi wa Bodi ya TPA.

\"\"

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TPA.

\"\"

Baadhi ya Wageni kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia.

_____________________________________________

Ziara ya Mafunzo Bandari ya Dar es Salaam

Machi, 2017:

Wanafunzi wa \'St. Claver High School\' iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma wamepata fursa ya kuitembelea Bandari ya Dar es Salaam kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji.

 

\"\"

Afisa Mawasiliano Mwandamizi Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Levina Msia akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Bandari kwa Wanafunzi hao wakati wa ziara hiyo.

\"\"

Picha ya pamoja na baadhi ya Menejimenti ya Bandari ya Dar es Salaam.

______________________________________________________

Spika wa Bunge atembelea Bandari ya Dar es Salaam

Machi, 2017:

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai leo ameongoza baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Bunge za Bajeti, Nishati na Madini katika Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea makontena yenye mchanga wa dhahabu ambayo yamezuiliwa bandarini na kwenye Bandari Kavu ya Mofed.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Spika alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit C.V. Kakoko.

\"\"

 Mhe. Job Ndugai akiwa katika ziara hiyo ya Bandari ya Dar es Salaam.

\"\"

 Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) akiwa pamoja na Wabunge kwenye ziara hiyo.

\"\"

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ziara ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Job Ndugani, Bandari ya Dar es Salaam.

\"\"

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko wakijadiliana jambo wakati wa ziara hiyo ambayo imefanyika hivi karibuni.

\"\"

 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua matukio mbalimbali ya ziara ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

 ___________________________________________________________

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuufahamisha umma kwamba imebaini makontena mengine 256 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika Bandari Kavu ya MOFED iliyopo Kurasini, jijini Dar es Salaam yakisubiri kukamilisha taratibu za kiforodha kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia Kitengo cha Makontena kinachoendeshwa na kampuni binafsi(private) ya TICTS.


Makontena hayo ambayo tayari yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo Kampuni ya Wakala wa Forodha ijulikanayo kwa jina la Freight Forwarders Tanzania Ltd iliyopo Dar es Salaam ilikuwa katika hatua za mwisho  kukamilisha taratibu za kiforodha kusafirisha mzigo huo.


Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 23.3.2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alitembelea bandari ya Dar es Salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa dhahabu kutoka katika migodi mbalimbali inayochimba madini nchini Tanzania.


Mhe. Rais aliagiza kuzuiliwa kwa makontena hayo bandarini na kuwekwa chini ya ulinzi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama Bandarini hadi hapo Serikali itakapoelekeza vinginevyo. Makontena hayo yote yapo chini ya uangalizi wa vyombo vya dola bandarini.


Makontena hayo 256 yaliyozuiliwa leo ni kama ifuatavyo;
-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 180 ilipokelewa tarehe 17/12/2016 ikitokea katika migodi ya BUZWAGI  ikiwa na jumla ya makontena 20.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 181 ilipokelewa tarehe 23/12/2016 ikitokea katika migodi ya BUZWAGI  ikiwa na jumla ya makontena 20.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 182 ilipokelewa tarehe 26/12/2016 ikitokea migodi ya BUZWAGI ikiwa na jumla ya makontena 20.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 183 ilipokelewa tarehe 3/1/2017 ikitokea migodi ya  BUZWAGI ikiwa na jumla ya makontena 15.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI 194 ilipokelewa tarehe 4/1/2017 ikitokea migodi ya PANGEA MINE ikiwa na jumla ya  makontena 22.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 184 ilipokelewa tarehe 23/1/2017 ikitokea migodi ya  BUZWAGI ikiwa na jumla ya makontena 20

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI 195 ilipokelewa tarehe 26/1/2017 ikitokea migodi ya PANGEA MINE ikiwa na jumla ya makontena 22.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 185 ilipokelewa tarehe 27/1/2017 ikitokea migodi ya  BUZWAGI ikiwa na jumla ya makontena 20.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI 195 B ilipokelewa tarehe 29/1/2017 ikitokea migodi ya PANGEA MINE ikiwa na jumla ya makontena 22.

-    Namba ya kusafirishia mzigo MRI BUZ 186 ilipokelewa tarehe 25/2/2017 ikitokea migodi ya  BUZWAGI ikiwa na jumla ya makontena 20.

-    Namba ya kusafirishia mzigo CLI BUL/001 ilipokelewa tarehe 26/2/2017 ikitokea migodi ya PANGEA MINE ikiwa na jumla ya makontena 18.

-    Namba ya kusafirishia mzigo PCC 060 B ilipokelewa tarehe 3/3/2017 ikitokea migodi ya PANGEA MINE ikiwa na jumla ya makontena 20.

-    Namba ya kusafirishia mzigo CLI BUZ 006 ilipokelewa tarehe 4/3/2017 ikitokea migodi ya PANGEA MINE ikiwa na jumla ya makontena 17.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuuhakikishia umma kwamba kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, itaendelea kudhibiti usafirishaji holela wa rasilimali za nchi kwa kuzingatia maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania( TPA)
 

____________________________________________________________________________

Waziri Makamba akagua athari za Mazingira Tanga

Machi, 2017:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) ametembelea Kisiwa cha Toten (ambacho kinapakana na Bandari ya Tanga) kuangalia athari za mmomonyoko wa fukwe katika eneo hilo na hatua za kuchukua. Mmomonyoko wa fukwe katika eneo hilo umesababishwa na changamoto kubwa zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi zinazopelekea maeneo ya nchi kavu yanayopakana na bahari kulika na maji kutokana na kuinuka kwa kina cha bahari.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara yake katika eneo la Raskazoni kwa sasa bahari inakula eneo la nchi kavu karibu kabisa na barabara pamoja kisiwa cha wafu/kifo (Toten Island) ambacho kipo hatarini kupotea kutokana na kuinuka kwa kwa kina cha maji. Waziri Makamba alipata wasaa wa kutembelea na kukagua maeneno yanayotajwa kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ya Raskazoni pamoja na kiswa hicho ambapo ameahidi kutuma wataalamu watakaoshirkiana na wataalamu waliopo mkoani Tanga ambao baada ya kufanya upembuzi yakininifu watapendekeza hatua bora zaidi za kuchukua kukabiliana na changamoto hiyo.

Vilevile ameagiza kufanyika operesheni maalum ya kupambana na wavuvi haramu wananaotumia baruti katika uvuvi jambo lenye athari kubwa sana mazingira ikiwemo kuua na kuharibu matumbawe ambayo ni moja ya tegemeo kubwa kwa mazalia ya samaki na ambayo huchukua mpaka miaka 70 kurudi hali yake baada ya uharibifu. Waziri Makamba ameanisha umuhimu wa kuchukua hatua za haraka katika kukiokoa kisiwa cha Toten ambapo amesema hatua za haraka ni kujenga ukuta kama serikali ilivyofanya kwa sehemu za Dar es Salaam na Pangani.

 

Ameainisha kwa undani kuwa kisiwa hicho kina faida na umuhimu mkubwa sana kwa bandari ya Tanga, kisiwa hicho ndicho kinaikinga bahari ya Tanga dhidi ya mawimbi makubwa ya bahari ambayo hutua kwanza kisiwani hapo laikini vilevile taa za kuongozea meli zipo kisiwani pale lakini muhimu zaidi kulika kwa kisiwa hiki kunaongeza tope katika kina cha bandari ya Tanga jambo linalotishia thamani ya bandari hiyo. 
 
\"\"
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Donald Ngaile.
 
\"\"
 
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akipatiwa maelezo kutoka kwa Harbour Master, Bandari ya Tanga, Capt. Andrew Mattlya.
 
 
\"\"
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.)akiwa kwenye Tug Boat wakati wa ziara yake.
_______________________________________________________

Mwenyekiti wa Bodi ya TPA Akagua Miradi Bandari ya Tanga

Machi, 2017:

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Prof. Ignas Rubaratuka amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi katika Bandari ya Tanga ili kujiridhisha na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Bandari hiyo. Katika ziara hiyo Prof. Rubaratuka aliongozana na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu, (Miundombinu), Eng. Karim Mattaka.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Gati Na. 2, Ujenzi wa Gati la Kupakulia Mafuta eneo la Raskazone na Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Bomba la Mafuta litakalotoka Hoima nchini Uganda mpaka eneo la Bandari ya Tanga.

\"\"

 Prof. Rubaratuka akitoa maelezo kwa Watendaji wa Bandari ya Tanga kuhusiana na utekelezaji wa miradi katika Bandari hiyo.\"\"

Prof. Rubaratuka akipatiwa maelezo kuhusiana na ukarabati wa Gati la Mafuta katika eneo la Raskazone.

\"\"

Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Donald Ngaile akitoa maelezo kwa Prof. Rubaratuka na ujumbe wake kuhusiana na ukarabati wa Gati namba 2.

\"\"

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu), Eng. Karim Mattaka akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Bandari ya Tanga.

\"\"

Prof. Rubaratuka akipokea maelezo kutoka kwa Harbour Master, Capt. Andrew Mattlya (wapili kushoto) kuhusiana na eneo la Chongoleani ambapo kutajengwa matanki na Gati la mafuta ghafi yatakayo safirishwa kutoka Hoima nchini Uganda.

\"\"

Prof. Rubaratuka akishuhudia ukarabati wa Gati na 2 ukiwa unaendelea katika Bandari ya Tanga.

___________________________________________________

Wajumbe Bodi ya TPA waongezewa Ujuzi!

Machi, 2017:

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA wanahudhuria mafunzo maalumu yanayolenga kuwaongezea ujuzi na weledi katika kutimiza majukumu yao kama Wakurugenzi wa Bodi.

Katika mafunzo hayo ya siku mbili, Wakurugenzi hao watapitia mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya utawala bora, wajibu wa Bodi, majukumu ya Mwenyekiti, Mtendaji Mkuu na Maafisa Waandamizi ndani ya Taasisi.

Mbali na hayo Wajumbe hao pia watapatiwa mafunzo maalumu kuhusiana na umuhimu wa Kamati za Bodi na namna ya kutathimini utendaji wa Bodi (Board Self Assessment)

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Wataalam kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania na yatakamilika tarehe 12 Machi, 2017. Bodi ya TPA yenye Wakurugenzi nane wenye fani mbalimbali inaongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Ignas Rubaratuka ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

\"\"

Katika Picha: Wakurugenzi wa Bodi ya TPA, wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu kutoka Taasisi ya Wakurugenzi. Katikati waliokaa ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Ignas Rubaratuka na wapili kulia ni Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko.

___________________________________________

Rais Magufuli azindua rasmi Ujenzi wa Gati Bandari ya Mtwara Leo!

Machi, 2017:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameweka rasmi jiwe la msingi kwenye Bandari ya Mtwara, kuashiria kuanza kwa Ujenzi wa Gati Jipya Na. 2 katika Bandari hiyo litakalokuwa na urefu wa mita 350!

Yafuatayo ni Matukio mbalimbali katika picha kuhusiana na uwekaji huo wa jiwe la msingi, tukio ambalo limefanyika leo Jumamosi, Machi 04, 2017 katika Bandari ya Mtwara.

 

\"\"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Wadau mbalimbali wakati hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara leo.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB), akisoma hotuba yake wakati wa hafla hiyo.

\"\"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizindua rasmi jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara leo.

\"\"

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akitoa maelezo kwa Mhe. Rais kuhusiana na mradi wa ujenzi wa Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara leo.

\"\"

Mhe. Rais akishuhudia, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mwakilishi kutoka Kampuni itakayojenga Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara wakitia saini makubaliano ya kuanza kwa ujenzi huo leo.

\"\"

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Dkt. Francis Michael (wanne kulia) akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi hiyo kutoka kulia ni Bw. Aziz Kilonge, Bw. Jaffer Machano, Bi. Jayne Nyimbo, Dkt. Jabir Kuwe na Bw. Renatus Mkinga wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara

\"\"

Baadhi ya Watumishi wa TPA kutoka katika Bandari mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 leo.

\"\"

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Francis Michael wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara

________________________________________________________

MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ATAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA GATI BANDARI YA MTWARA LEO!

Machi, 2017:

 

\"\"

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

 

Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inapenda kuwatangazia Wananchi wa Manispaa ya Mtwara - Mikindani Mkoa wa Mtwara na Mikoa Jirani kwa Ujumla kwamba TPA inatarajia kujenga Gati Na. 2 ambalo ni jipya la mita 350 Bandari ya Mtwara.

Ujenzi huo utaongeza sana uwezo wa kuhudumia shehena kubwa zaidi kama vile Simenti kutoka Kiwanda cha Dangote, Makontena na Mafuta kwa kutumia meli kubwa na nyingi zaidi.

Ili kuwawezesha Wananchi kushuhudia azma hiyo, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Gati hilo leo asubuhi Jumamosi tarehe 4 Machi 2017.

Kabla ya kuweka jiwe la msingi Mheshimiwa Rais akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Viongozi mbalimbali na Wananchi mtashuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko akiweka saini kwenye mkataba pamoja na Wakandarasi wa Mradi huo na kisha kupata maelezo ya mradi.

Wote mnakaribishwa kuanzia saa 2 asubuhi kwa kuwa huu sasa ni wakati wa Mtwara.

Mnaombwa kupita Geti Na. 3.

___________________________________________________________________________________

SERIKALI YA CHINA YAKABIDHI \'SCANNER\' KWA BANDARI ZA DAR ES SALAAM NA TANGA

 

Machi, 2017:

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia ubalozi wake hapa nchini imekabidhi rasmi mashine mpya ‘scanner’ (gantry & mobile) mpya za ukaguzi wa mizigo zitakazotumiwa na Bandari za Dar es Salaam na Tanga kudhibiti mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti mizigo haramu kama vile pembe za ndovu, mihadarati na bidhaa nyingine haramu.

Tukio la makabidhiano hayo limefanyika ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, Machi 01, 2017 mbele ya wageni na wadau mbalimbali wa Bandari ikiwamo Mamlaka ya Usimamizi wa Mapato Tanzania (TRA).

Makabidhiano hayo yamefanyika baina ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) na Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deudedit Kakoko na Wajumbe wengine wa Bodi ya Mamlaka, Dkt. Francis Michael, Dkt. Jabiri Bakari, Bi. Jayne Nyimbo na Bw. Renatus Mkinga.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Lu Youqing wakiweka saini hati za makabidhiano ya Scanner zilizotolewa na Serikali ya China kwa Bandari za Dar es Salaam na Tanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) na Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing wakibadilishana nyaraka za makabidhiano za scanner mpya za kukagua mizigo bandari ya Dar es Salaam na Tanga hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko.

\"\"

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (kulia) akisoma hotuba yake wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya scanner za ukaguzi wa mizigo hivi karibuni.

\"\"Prof. Mbarawa akikata utepe kuzindua rasmi matumizi ya scanner za mizigo huku Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka, Wajumbe wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko wakishuhudia.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) akipewa maelezo ya uendeshaji wa scanner mpya na Meneja Mradi Bw. Mtani Rugina.

\"\"

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (wapili kulia) akikabidhi zawadi maalumu ya picha ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing ikiwa ni ishara ya kuishukuru Serikali ya China kwa mchango wake wa kuziendeleza Bandari za Dar es Salaam na Tanga.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TPA.

\"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dowuta Taifa, Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi wa TPA wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya scanner mpya za ukaguzi wa mizigo.

_______________________________________________________________________________________

 

ZIARA YA MWANAMFALME WA SAUDI ARABIA BANDARI YA DAR ES SALAAM

 

Februari, 2017:

\"\"

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Freddy Liundi (watatu kulia) akifafanua jambo kwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Ahmed Ben Bendar Alsedary  (wapili kushoto) wakati wa ziara yake bandari hivi karibuni.

 

\"\"

Mhandisi, Joseph Mtenga (kulia) akitoa maelezo kwa Mwanamfalme kuhusu shughuli mbalimbali za kitengo cha mafuta cha KOJ kilichopo bandarini hapo.

\"\"

 

________________________________________________________________________________

 

TPA TO CONSTRUCT A TZS 7 BILLION INLAND PORT IN NINE WEEKS

 

February, 2017:

 

Minister for Works, Transport and Communication, Hon. Prof Makame Mbarawa said the government through TPA will next month start construction of a seven billion shillings inland container depot (ICD) at Ruvu area in Coast Region.

 

Makame Mbarawa, said the ICD will be constructed in 500 hectares of land and will be completed in nine weeks.  He was speaking after he had witnessed the signing of an agreement to implement the ICD project between the Tanzania Ports Authority (TPA) and Suma JKT of the Tanzania National Services.

_________________________________________________________________________________

SUMA JKT KUJENGA BANDARI KAVU ENEO LA RUVU KWA WIKI TISA!

 Februari, 2017

TPA imeingia makubaliano na Shirika la kiuchumi la Jeshi la Kujenga Taifa SumaJKT, ya kujenga Bandari Kavu katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani na kuukamilisha ndani ya Wiki Tisa (9).  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amesena ujenzi huo anaotarajiwa kugharimu takribani Shilingi Bilioni 7.286 utapunguza kwa kiasi kikubwa foleni ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Bandari Kavu hiyo inatarajiwa kujengwa kwenye eneo la takribani hekta 500. Kwa upande wake mwakilishi wa mshauri kutoka SUMAJKT, Bw. John Mbungo amesema wanao uwezo wa kukamilisha kazi hiyo ya ujenzi ndani ya wiki tisa kwa vigezo na viwango vyote vinavyohitajika.

 

 \"\"

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (kulia) na Mwakilishi wa SumaJKT, Bw. John Mbungo (kushoto) wakitia saini nyaraka za makubaliano ya ujenzi.

 \"\"

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (kulia) na Mwakilishi wa SumaJKT, Bw. John Mbungo (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya ujenzi.

 \"\"

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza wakati wa shughuli ya uwekaji saini.

__________________________________________________________________________________


Port of Dar is Tanzania’s rudder for economic development

February, 2017

It is probably, now more than ever the perfect time for Port of Dar es Salaam, to expand its territory to hold more cargo volume and create new transport links. With all these developments, they will turn Tanzania to a regional hub, more of the same to be dubbed as the Dubai of East Africa, according to reports.

“The Dar es Salaam port is an engine for economic growth, if we invest in logistic centers, improve on infrastructure and create a facilitative environment, we can easily turn Dar es Salaam into another Dubai of its kind in East Africa,” said Tanzania China Mining Association Chairman Superintended Andrew Huang.

The fifth phase government under Dr. John Pombe Magufuli has a chance to use effectively the Dar es Salaam port to increase 100% of the country source of revenue to foster the city to become a Dubai of the East Africa region.

Andrew Huang said the measures taken by President Magufuli have removed bureaucratic hurdles hence promote cargo volumes from neighboring countries and abroad.

He said it is easy to attract all large investors and make Dar es Salaam a huge financial center by allowing and encouraging colossal banks to invest and conduct financial business and market in the country.

Huang noted the city of Dar es Salaam deserved to have well-constructed roads, railways to the central line, buildings, malls and fast track it as a satellite city ready for massive investment from international business people.

Tanzania, just like its neighbor Kenya, wants to capitalize on a long coastline and upgrade existing rickety railways and roads to serve growing economies in the land-locked heart of Africa from Uganda on its north border to Malawi in the south.

But for sometimes the pace of progress had been held back by red tape, while experts said existing transport links were crumbling or inefficient, including the Dar es Salam port where vessels often wait days to dock, driving up costs to importers.

According to the International Association of Ports and Harbors, it is the fourth largest port on the African continent’s Indian Ocean coastline after Durban, Mombasa, and Maputo.

The port acts as a gateway for commerce and trade for Tanzania and numerous bordering landlocked states and for years the inefficiencies at the port has cost the regional economy millions of dollars; in 2012 the total global welfare loss caused by the inefficiencies of the port stood at $1.8 billion for the Tanzanian economy and $830 million for the neighboring countries.

Tanzania’s largest commercial city Dar es Salaam one of the fastest-growing in Africa has redrawn its master plan to try to become a megacity prepared for climate change, and not a city of worsening urban sprawl and flooding.

The plan, which looks ahead to 2036, aims to transform the city of over 4.5 million people and proposes creation of a Metropolitan Development Authority to oversee planning and major infrastructure development, including transportation and utilities.

Source: The Exchange

__________________________________________________________________________________

Waziri wa Nishati na Maji wa Zambia atembelea boya la SPM

Bandari ya Dar es Salaam

Februari, 2017

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Maji wa Zambia, Mheshimiwa David Mabumba wameipongeza Bandari ya Dar es Salaam kwa huduma nzuri inazozitoa katika kuhudumia mzigo za Zambia hususan Mafuta. Pongezi hizo wamezitoa wakati wa ziara yao ya kutembelea Boya la Single Point Mooring (SPM) eneo la Mji Mwema ambalo linatumika kupakulia mafuta ghafi kwa ajili ya Zambia. Mafuta ghafi hayo husukumwa kupitia bomba la TAZAMA mpaka Ndola Zambia.

Ziara hiyo wameifanya kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na Mheshimiwa Edgar Lungu wa Zambia ya kufuatilia utendaji wa Bomba la TAZAMA ili kuangalia namna ya kuboresha utendaji wake kwani bomba hilo ni muhimu kwa uchumi wa Zambia kwani ndilo linalotumika kusafirishia mafuta yanayotumika nchini humo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Deusdedit Kakoko amewaahidi Mawaziri hao kwamba Bandari ya Dar es Salaam itaendelea kutoa huduma bora kwa mzigo wa Zambia ili Wazambia waendelee kutumia bandari hiyo.

\"\" 

Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko ( wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Nishati na Maji wa Zambia,  Mh. David Mabumba wa Zambia (wa saba kutoka kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Mh. Prof. Sospeter Muhongo (wa nane kutoka kushoto)  baada ya kutembelea Boya la SPM.

\"\"

Mh. Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia) akielezea jambo kwa Mhe. David Mabumba (wa tatu kutoka kushoto) na Mhandisi Deusdedit Kakoko (wanne kutoka kulia) wakiwa ndani ya Tug kutembelea Boya la SPM.

\"\"

Mhandisi Deusdedit Kakoko akiwa anamuonyesha kitu kwenye ipad Harbour Master wa TPA, Capt. Abdullah Mwingamno.

\"\"

Boya la SPM pembeni yake ni Boti ya ulinzi.