Pic 4

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omar Mgumba (MB) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na baadae kufanya ziara bandarini kwa lengo la kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam leo Ijumaa, Septemba 21, 2018.

Pic 1

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omar Mgumba (MB) akimsikiliza Naibu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam (Utekelezaji) Bw. Ahmed Mchalaganya (kulia) akitoa maelezo kuhusiana na namna TPA inavyohudumia shehena ya mizigo inayopita bandarini hapo wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao kilichopo ndani ya Bandari ya Dar es Salaam.

Pic 2

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omar Mgumba (MB) akitoa maelekezo kwa maofisa wa kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini wakati wa ziara yake Bandari ya Dar es Salaam kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho bandarini.