TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwataarifu waombaji kazi waliotuma maombi ya kujaza nafasi wazi sitini na nane (68) za kada mbalimbali zilizotangazwa kupitia  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa Tangazo lenye Kumb.Na:EA.7/96/01/J/22 lilitolewa kuanzia tarehe 26 Novemba, 2018 kuwa, Orodha ya Waombaji waliofuzu kuitwa kwenye usaili inapatikana kwenye tovuti za Sekretarieti ya Ajira na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari.

Aidha, kwa Waombaji  wa nafasi za Menejimenti waliofuzu kuitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia barua pepe zao  zilizowasilishwa wakati wa maombi ya kazi na kwa njia ya simu zao.

Zoezi la usaili litaanza tarehe 3 Januari, 2019 na kumalizika tarehe 18 Januari, 2019. Waombaji mlioitwa kwenye usaili mnatakiwa kuhudhuria usaili huo kwa tarehe na muda  mliopangiwa kwenye tangazo.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari inawatakia maandalizi mema ya usaili huo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

Bandari Tower – One Stop Centre

Kiwanja Na. 1/2, Sokoine Drive

S.L.P 9184

11105 DAR ES SALAAM