WAZIRI MKUU KUTEMBELEA BANDARI YA MTWARA LEO OKTOBA MOSI!

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) anatarajiwa kutembelea Bandari ya Mtwara leo Oktoba 1, 2019 kwa lengo la kukagua shughuli za Bandari hiyo.

Katika ziara yake Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea Bandari ya Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine atakagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara.

Ziara hiyo imeelezwa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko wakati akifungua kikao cha 26 cha Baraza kuu la Wafanyazi wa TPA kinachofanyika mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Katika hatua nyingine Eng. Kakoko amepongeza Menejimenti ya TPA, DOWUTA pamoja na Wafanyakazi wa TPA kwa ushirikiano wanaoonesha kwa kufanya kazi kwa bidii na kuongeza tija na ufanisi ndani ya Mamlaka.

DSC 0057

DSC 0047

DSC 0053

DSC 0042