Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), ametembelea Bandari ya Mtwara na kukagua jinsi ambavyo usafirishaji wa Korosho kwenda nje ya nchi unavyoendelea.

Sambamba na ukaguzi huo Waziri Mkuu pia ameipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kupitia Bandari ya Mtwara kwa jinsi ambavyo inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha korosho hizo zinasafirishwa kwa ufanisi ambapo pia ametoa maagizo mbalimbali kuhusiana na usafirishaji na uwekezaji wa zao hilo la Korosho nchini.

Mara baada ya ziara hiyo ya Waziri Mkuu Bodi ya TPA ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Ignas Rubaratuka ilifanya ukaguzi mradi wa ujenzi na upanuzi wa Bandari ya Mtwara na kuiagiza Menejimenti ya TPA kuhakikisha maagizo ya Waziri Mkuu pamoja na ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Katika picha ni matukio mbalimbali kuhusiana na ziara ya Waziri Mkuu iliyofanyika Oktoba 1, 2019.

MKURUGENZI MKUU AKITOA MAELEZO YA NAMNA SHEHENA YA KOROSHO INAVYOHUDUMIWA

Mhe. Waziri Mkuu akisisitiza jambo na kutoa maagizo kwa Menejimenti ya TPA kuhusiana na kuhudumia zao la Korosho ndani ya Bandari.

MH WAZIRI MKUU AKIANGALIA UPAKIAJI WA KOROSHO KWENYE MELI

Mhe. Waziri Mkuu akiangalia upakiaji wa Korosho Melini.

MKURUGENZI MKUU MHANDISI D C V KAKOKO AKITOA MAELEZO KWA WAZIRI MKUU

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akimpa ufafanuzi Waziri Mkuu kuhusiana na kazi ya upakiaji Korosho ndani ya Meli.

MWENYEKITI WA BODI AKIMKARIBISHA WAZIRI MKUU BANDARINI MTWARA

Mhe. Waziri Mkuu akikaribishwa Bandari ya Mtwara na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka.

WAZIRI MKUU AKIANGALIA USAFIRISHAJI WA KOROSHO

WAZIRI MKUU ALIPOFANYA ZIARA BANDARINI MTWARA

Waziri Mkuu akiwa ndani ya Bandari ya Mtwara kukagua shughuli mbalimbali za kusafirisha zao la Korosho.

MWENYEKITI WA BODI AKITOA MAELEKEZO KWA MKURUGENZI MKUU

Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko.

MWENYEKITI WA BODI NA MKURUGENZI MKUU WALITEMBELEA BANDARI YA MTWARA KUKAGUA MAENEO YA BANDARI IKIWEMO UJENZ WA GATI YA NYONGEZA UNAOENDELEA

Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (kushoto) pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Bodi wakiwa Bandarini kukagua shughuli za uendeshaji sambamba na ujenzi na upanuzi wa Bandari. Kulia ni Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara.