MKUU WA MKOA WA MOROGORO AZINDUA MICHEZO YA BANDARI 2019!

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Ole Sanare amezindua michezo ya 13 ya Bandari maarufu kama "Bandari Inter-Ports Games 2019".

Michezo hiyo ya Bandari imeanza kutimua vumbi Oktoba 14 katika uwanja wa Jamhuri pamoja na viwanja vya JKT bwalo la Umwema.

Akizungumza kabla ya uzinduzi, Mhe. Sanare amewaasa Wanamichezo kutumia michezo hiyo kuongeza ari na hamasa katika kuhudumia wateja wa Bandari ili kuliongezea Taifa mapato sambamba na kuunga mkono kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambae pia amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Bandari zinajiendesha kwa ufanisi na tija.

Mapema akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya HR ya TPA, Bi. Jane Nyimbo amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla kwamba TPA itaendelea kusimamia maadili na ufanisi katika kazi na itatumia michezo hii kuwapa Wafanyakazi motisha, ari na hamasa ya kuchapa kazi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko ametoa pongezi kwa Uongozi wa Mkoa wa Morogoro kwa kutoa kibali cha kuruhusu michezo hiyo kufanyika na amewaasa Wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia miiko ya kazi na kanuni za kazi ambapo pia ametoa wito kwa Wafanyakazi kutumia michezo kama sehemu ya kuboresha afya zao, motisha na kuongeza tija ndani ya Mamlaka.

Michezo ya Bandari inafanyika mara moja kila mwaka ambapo katika kipindi cha miaka miwili mfululizo imefanyika katika Mkoa wa Morogoro, michezo hii kama ilivyokuwa mwaka mbali na kuzihusisha timu za vituo vya Makao Makuu, Bandari ya Mtwara, Tanga na Bandari za Maziwa pia kwa mwaka huu inazihusisha timu wageni kutoka Bandari Zanzibar pamoja na TICTS.

Katika michezo hii ya siku tano inayotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 18, 2019 takribani michezo nane itashindaniwa hii ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, pete, kikapu, kuvuta kamba, riadha, kurusha mkuki, kurusha tufe na mchezo mkongwe wa bao ambao Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alikuwa pia mchezaji.

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA SHIGHULI YA UFUNGUZI ILIYOFANYIKA OKTOBA 14, 2019.

DSC 0964

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Ole Sanare akizungumza na Wanamichezo wa Bandari.

DSC 0963

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo akizungumza na Wanamichezo.

DSC 0959

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya HR, Bi. Jane Nyimbo akizungumza na Wanamichezo.

DSC 0947

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akizungumza na Wanamichezo wa Bandari.

DSC 0943

Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala TPA, Bw. Gabriel Mwita akizungumza na Wanamichezo.

DSC 0960

DSC 0818

DSC 0821

DSC 0827

DSC 0828

DSC 0833

DSC 0836

DSC 0839

DSC 0844

DSC 0850

DSC 0856

DSC 0970

DSC 0972

DSC 0974

DSC 0978

DSC 0979

DSC 0982

Mkuu wa Mkoa akifunga goli kuashiria uzinduzi rasmi wa michezo.

DSC 0980

Mkurugenzi Mkuu wa TPA akionesha umahiri wake wa kumiliki mpira.

DSC 0983

DSC 0986DSC 0995DSC 0995DSC 0996DSC 0998DSC 1003

pi 1 1pi 1 2pi 1 3pi 1 4pi 1 5pi 1 6pi 1 7pi 1 8

pi 1 9pi 1 10pi 1 11pi 1 12pi 1 13pi 1 14pi 1 15pi 1 16pi 1 17pi 1 18pi 1 19pi 1 20pi 1 21pi 1 22pi 1 23pi 1 24pi 1 25