Bandari Ziwa Nyasa

Bandari kubwa zilizopo Ziwa Nyasa ni Mbamba bay na Itungi /kiwira. Bandari ya Kiwira imeanzishwa kama bandari ya shehena. Ina gati la kushukia na kupandia abiria, Bandari ya Kiwira ina mitambo ya kuhudumia shehena kama vile Winchi itembeayo, foko na Vinyakulio (grabs). Kwa sasa bandari hii ndio makazi ya Mv Ruvuma, Mv Njombe na Mv Mbeya ll zinazomilikiwa na TPA.

Program za Maendeleo

  • Kujenga gati Itungi, Mbamba Bay, Manda, Lupingu, Liuli na Matema katika Bandari ya Ziwa Nyasa.
  • Ununuzi vifaa vya kupakulia na mizani za kupimia mzigo uliopakiwa kwenye magari.

Miundombinu

  • Gati, maghala, eneo la kuhudumia abiria na maeneo ya wazi ya kuhifadhia mizigo

Vifaa vya bandarini

  • Meli mbili zenye uwezo wa kubeba uzito wa tani zametriki 1000 kila moja na meli moja ya abiria na mizigo inayoweza kusafirisha abiria 200 na mizigo ya tani za metriki 200.
  • Winchi inayotembea
  • Foko
  • Mizani

Miradi Iliyotekelezwa

  • Ukarabati wa Bandari ya Itungi
  • Utengenezaji wa maeneo ya abiria/shehena katika Bandari ya Kiwira
  • Ukarabati wa bandari ya Mbamba bay
  • Uendelezaji wa bandari ya Ndumbi
  • Ujengaji wa maeneo ya kupandia na kushukia abiria bandari mbalimbali wanakofikia.

Bandari Nyengine zilizoko ziwa nyasa

BANDARI YA MBAMBA BAY

Maelezo ya ziada

Bandari ya Mbamba bay ina Gati linalofaa kwa mizigo midogo. Bandari itaendelea kuboreshwa kutokana na kujengwa kwa meli mpya pia uendelezaji wa Ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor).

BANDARI YA NDUMBI

Maelezo ya ziada

Bandari ya Ndumbi ina Gati, maghala, ofisi, eneo la wazi na sehemu ya kuhudumia abiria. Bandari ya Ndumbi imeonekana kuwa bandari muhimu sana iliyojengwa kimkakati kwa usafirishaji wa makaa ya mawe kwenda Bandari ya Kiwira na Bandari za Malawi kama vile Monkey bay na Chipoka

BANDARI YA ITUNGI

Maelezo ya ziada

Bandari ya Itungi imelengwa kuwa kituo cha abiria kitakacho shughulikia shehena ndogo ndogo. Bandari hii inagati lenye urefu wa mita 70, ni ofisi kuu ya Bandari za ziwa Nyasa. Inakadiliwa na tatizo la mchanga wa tope unaothiri njia ya kuingilia Bandarini hata hivyo utaratibu wa kudhibiti unaonesha mafanikio . Bandari ina mtambo wa kusafisha taka chini ya maji naa hivyo kuwezesha kina cha maji kuongezeka katika mkondo wa kuingilia upande wa Gati.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Meneja wa Bandari Ziwa Nyasa,
Mamlaka ya Bandari (TPA),
S.L.P 400,
Kyela, Tanzania

Simu: +255 (0) 786 364 622
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.