Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeng’ara katika maonyesho ya 18 ya biashara ya Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni baada ya kutwaa tuzo ya mshindi wa jumla. Katika maonyesho hayo, TPA pia imeibuka mshindi wa kwanza kwa Taassi za Serikali Kuu na Mitaa, Idara na Wakala, Huduma za Serikali/Wakala wa Taasisi na mshindi wa kwanza kwenye kipengele cha Muonyeshaji Bora wa maonyesho kwa upande wa Tanzania. , ,