Sélectionnez votre langue

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Ellinami Minja,wamefanya Ziara nchini Burundi ili kuona kazi zinazofanywa na Ofisi ya TPA nchini humo.

Katika Ziara hiyo, wamepata nafasi ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi ambapo walipokelewa na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa juu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Burundi, ambapo TPA ni mdau muhimu katika kuimarisha mahusiano hayo kupitia Sekta ya Uchukuzi.

Wajumbe wa Bodi pia wameonana na wateja wa TPA nchini Burundi na kupata maoni yao kuhusu Ufanisi wa TPA katika kuhudumia Shehena inayokuja nchini humo pamoja na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Uchukuzi wa Wizara ya Uchukuzi ya Burundi Bw. Athanase Ndayirigire  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari ya Bujumbura (AMPB) Bi. Godeliève Nininahazwe.

Contactez-nous

Pour toute question ou assistance, contactez-nous 24h/24 et 7j/7.
0800-110032
P.O Box 9184 Dar es salaam
dg@ports.go.tz
255 22 2130390

Nouvelles Burundi

WAJUMBE WA BODI YA TPA KWENYE ZIARA NCHINI BURUNDI

3 Février 2025

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Ellinami Minja,wamefanya Ziara nchini Burundi ili kuona kazi zinazofanywa na Ofisi ya...
  Dis m'en plus