Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko tarehe 26 na 27 Januari, 2019 amekutana na kufanya mikutano na Wadau wa bandari katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na wadau wa bandari wa Mkoa wa Arusha, Mhandsi Kakoko amesema kuwa lengo la kukutana na wadau hao ni kuwafahamisha maboresho mbalimbali yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika bandari ya Tanga na kuifanya bandari hiyo kutoa huduma bora zaidi

Mhandisi Kakoko aliongeza TPA inalenga kutumia mikutano na wadau kupata mrejesho ya huduma zinazotolewa na bandari na maeneo gani huduma zinapaswa kuboreshwa

Katika kutatua changamoto zilizotolewa na wadau hao, Mhandisi Kakoko amesema kuwa changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wa TPA zitapatiwa ufumbuzi mara moja na zile ambazo zinahusu taasisi nyingine kama TRA,TBS, n.k atashirikisha watendaji wakuu wa taasisi hizo ili kuhakikisha mteja anayepita na kutumia bandari za Tanzania anapata huduma bora zinazolenga kumpunguzia mteja gharama ya kufanya biashara.

Kwa upande wake Meneja bandari ya Tanga Bw Percival Salama amewataka Wadau hao kutumia bandari ya Tanga katika kupitisha mizigo yao kutokana na kuhudumia wateja kwa kasi kubwa na haraka zaidi pamoja na kuwa na vifaa vipya vya kupakia na kupakua mizigo .

Mkutano wa wadau katika Mkoa wa Arusha ulifunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo na ule wa Mkoa wa Kilimanjaro ulifunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa Mhe.Mhandisi Aisha Amour.

WADAU

WADAU 1

WADAU 2

WADAU 3

WADAU 4

WADAU 5

WADAU 6

WADAU 7

WADAU 8