WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI BANDARI YA KIWIRA KYELA!

Jumamosi, Julai 29, 2017: Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja.

Meli hizo zimejengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine na zitatumika katika bandari za Kyela mkoani Mbeya.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ya Kyela kuwa walinzi wa meli hizo ambazo zinatarajiwa kutatua changamoto ya usafirishaji wa mizigo katika ziwa Nyasa na kuzitunza kwa maslahi mapana ya Taifa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TPA, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu), Mhandisi Karim Mattaka amesema ujenzi wa meli hizo zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja umekamilika kwa ufanisi mkubwa.
Mbali na kukamilika kwa meli hizo, TPA pia imeipa zabuni Kampuni ya Songoro Marine ya kuunda meli ya abiria na mizigo ambayo itakamilika hivi karibuni.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa .Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa  na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited.
Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt.  Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri   Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. Watatu kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Kyela Bw. Ajuaye Msese. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipatiwa maelezo na Harbour Master wa TPA, Capt. Mwingamno.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitizama mojawapo kati ya vyumba vya kupumzikia Mabaharia wa Meli hizo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipatiwa maelezo ya chumba cha mitambo 'engine' ya uendeshaji wa Meli hizo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Kyela ndani ya mojawapo kati ya Meli alizozindua.

Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira Wilayani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Karim Mattaka na Mkuu w Bandari ya Kyela, Bw. Ajuaye Msese wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa TPA na Manahodha wakati wa uzinduzi huo.

 

Meli mbili zilizonunuliwa na TPA zikiwa kwenye gati la bandari Kiwira Wilayani Kyela kabla ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuuu.