Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko amefungua kikao kazi cha 24 cha Kamati ya Utendaji ya Baraza kuu la Wafanyakazi kinachofanyika mjini Bagamoyo na kuwaasa Wajumbe kuwasilisha hoja na ushauri kwa usahihi na uwazi ili zijadiliwe kwa pamoja na hatimaye kufanyika maamuzi ya kuipeleka TPA mbele.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Baraza kuu la Wafanyakazi wametakiwa kuzingatia kwamba kikao hicho ni muhimu kwa maslahi ya TPA hivyo ni vyema mapendekezo yatakayowasilishwa yawe sahihi ili kuleta matokeo chanya katika kushughulikia changamoto mbalimbali.
“Kikao hiki ni muhimu sana pengine kuliko vikao vingine kwa kuwa ndicho kinachotoa ushauri na mapendekezo na hatimaye kuweza kuyatekeleza kwa nia ya kusonga mbele kwa ufanisi,” amebainisha Eng. Kakoko.
Kakoko amewaasa Wakurugenzi wa TPA kuwa makini na hoja za kikao na kutoa taarifa kamilifu, sahihi na za wakati wa sasa ili hatimaye zipokelewe na kujadiliwa n.a. wajumbe kwa maslahi ya TPA na Taifa kwa ujumla.