Meli ya Makasha RHL CALLIDITAS yenye urefu wa mita 260 na uapana a mita 37 huku ikiwa na kina mita 9 kwenda chini, yenye namba za Usajili IMO 9495777, kama inavyoonekana pichani ikiwa inaingia katika Bandari ya Dar es Salaam na kwenda moja kwa moja katika kitengo cha kuhudumia makasha TICTS,
Akiongea mara baada ya kufiikiwa kuingiza meli hiyo katika gati Bandari ya Dar es Salaam Capt. Abdul Mwingamno amesema kuwa huo na mwendelezo wa ujio wa mweli kubwa katika bandari ya Dar es Salaam ambapo hapo awali Bandari ilikuwa na uwezo wa kuhudumia meli isiyozidi urefu wa mita 234 .
Hatimaye hivi karibuni Tanzania ilishuhudia meli kubwa zilizo na urefu unaozidi mita 265 zikitia nanga katika bandari ya Dar es Salaam na kuondoa dhana ya kusema kwamba bandari kikomo chake ni kuhudumia meli isiyozidi urefu wa mita 234.
“Pamoja na maboresho yanayoendelea katika bandari ya Dar es Dar es Salaam leo tumefanikiwa tena kuingiza meli yenye urefu wa mita 260 na kuiingiza bandarini kiweledi na hatimaye kuendeleza uwezo wa Bandari katika kuhudumia meli kubwa ambazo kwa namna moja au ingize zinasaidia wasafirishaji katika kusafirisha mzigo mkubwa zaidi kwa wakati mmoja”. Alisema Mwingamno
Kwa upande wake Nahodha Mwandamizi Bw. Peter John ambaye ameingiza meli hiyo amewatoa hofu watumiaji wa bandari kwamba TPA imejidhatiti katika kutoa huduma bora zanye kiwango cha kimataifa huku akiwasisitizia watumiaji wa bandari kutumia bandari ya Dar es Salaam. “Bandari ya Dar es Salaaam kwa sasa usalama wa meli upo wa kutosha na marubani wanaujuzi na weledi uliotuka hvyo wasihofie na watumia bandari ya Dar es Salaam”. Alisema Peter.
RHL CALLIDITAS ilifanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na inatazamia kupakua makasha 644 TEUS na kupakia makasha 692 TEUS.