Mmoja wa Wafanyakazi wa TPA, Bi. Hilda Mwakatobe akikabidhi kwa mmoja wa wa Wazazi wa Watoto wagonjwa, Bi. Bi. Cheusi Selemani misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wao ambao wamezaliwa wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2019. Misaada hiyo imetolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TPA ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii hususani kuwafariji wazazi wa watoto hao.
Mmoja wa Wafanyakazi wa TPA, Bi. Zahara Malika akikabidhi kwa Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi Rehema Ally misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2019. Misaada hiyo imetolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TPA ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii hususani kuwafariji wazazi wa watoto hao.
Baadhi ya wanawake ambao ni wafanyakazi wa TPA wakiwasili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ili kuwatembelea na kuwapa misaada ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bi. Nuru Mhando (wapili kushoto) akimbeba mmoja wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi mara baada ya kuwakabidhi misaada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Baadhi ya Wanawake ambao ni Wafanyakazi wa TPA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na juice, biskuti, soda na fedha taslimu kwa ajili ya kulipia bima ya afya ya NHIF kwa watoto 20 wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo.