Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano TPA, Dkt. George Fasha, kulia, akifurahia jambo na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambapo alielezwa maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Mamlaka.
Na Leonard Magomba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), na kuelezwa maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.
Mara baada ya kuwasili kwenye banda hilo la TPA, Rais Samia alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano TPA Dkt. George Fasha na kupata fursa ya kuelezwa hatua mbalimbali za miradi ya maendeleo inayosimamiwa na TPA katika Bandari zake.
Mamlaka ya Bandari inasimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Bandari zake kote Nchini ikiwemo miradi ya kimkakati katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano TPA, Dkt. George Fasha, kulia, akifurahia jambo na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambapo alielezwa maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Mamlaka.
Mara baada ya kupojea taarifa ya TPA, Mhe. Rais alionekana kuvutiwa zaidi na utendaji wa Bandari ya Dar Es Salaam ambayo inazidi kupata mafanikio.
Rais Samia alitembelea banda la TPA mapema kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Wanawake na Vijana ulioandaliwa na Sekretarieti ya eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA).
Mkutano huo uliolenga kujadili mambo mbalimbali yahusuyo vijana na wanawake ulifanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 12 - 14 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.