Na Beatrice Jairo

Mabalozi wapya watatu wa Tanzania waendao Zimbabwe, Zambia na Uholanzi wamefanya ziara ya kimafunzo katika Bandari ya Dar es Salaam zenye lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za Bandari.

Mabalozi hao ambao ni Simoni Sirro anayekwenda Zimbabwe, Luteni Jenerali Methew Mkingule anayekwenda Zambia na Mhe Caroline Chipeta anayekwenda Uholanzi wamefanya ziara ya kimafunzo ili nao waende kuzitangaza Bandari hizo katika nchi wanazokwenda kufanyakazi.

Mara baada ya kufika Bandarini hapo, Mabalozi hao walipokekewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Juma Kijavara ambaye pamoja na mambo mengine, amewafahamisha namna mbalimbali za utendaji wa Bandari hiyo.

Amewaambia waheshimiwa Mabalozi kwamba Serikali imewekeza pesa nyingi katika kuboresha miundombinu ya Bandari hizo.

Alisema kwamba maboresho hayo yamezijengea uwezo mkubwa Bandari hizo katika kuhudumia mizigo na hatimaye kuweza kutoa huduma bora zaidi na kwa ufanisi.

Mwisho