Na Leonard Magomba

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imeshiriki maonyesho ya 3rd ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani huku ikiwahakikishia wadau wake upatikanaji wa huduma bora na za kisasa katika Bandari zake.

Akitoa maelezo kwa wadau mbalimbali waliotembelea Banda la TPA katika Maonyesho hayo, Kaimu Meneja Masoko wa TPA, Bw. Emmanuel Mrutu amesema wateja ni kipaumbele cha Mamlaka hivyo wamejipanga kuwapa huduma bora.

Bw. Mrutu ambaye alikuwa akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa Bandari waliotembelea Banda la TPA, alisema kwamba kuna uhusiano mkubwa kiutendaji kati ya shughuli za Bandari na wafanyabiashara.

Katika maonyesho hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani na kufunguliwa na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, yalienda sambasamba na kaulimbiu, “Pwani Sehemu Sahihi kwa Uwekezaji, kwa pamoja tujenge Viwanda kwa Ajira Endelevu.”

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi aliwasisitiza wawekezaji pamoja na wafanyabiashara kwenda kuwekeza katika Mkoa huo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw. Exaud Kigahe (Mb) alipotembelea Banda la TPA katika maonyesho hayo

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA, Bw. Leonard Magomba kushoto, akikabidhi tuzo iliyotunukiwa TPA kwa ushiriki wake katika maonyesho ya 3rd ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani kwa Meneja Mawasiiiano na Uhusiano, Bw. Nicodemus Mushi.

TPA ni moja ya taasisi za UMMA zilizowekeza katika Mkoa huo kwa kujenga Bandari Kavu ya Kisasa eneo la Kwala ambayo ina uwezo wa kuhifadhi Makasha na imeunganishwa na miundombinu ya Reli na Barabara.

Mwisho