Mhandisi Juma Kijavara akifungua mkutano huo
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuhudumia Shehena ya zao la Korosho kupitia Bandari ya Mtwara.
Mkakati huo uliobainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Pasduce Mbossa, ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa Mkutano wa Wadau wa Bandari kuhusu maandalizi ya usafirishaji wa zao la Korosho kupitia Bandari ya Mtwara, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Juma Kijavara amesema Bandari ya Mtwara ipo tayari kuhudumia shehena hiyo.
“Sisi kama TPA tumejipanga vizuri kabisa kuhudumia Shehena hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya Bandari ya Mtwara kusafirisha zao la Korosho.
Kama sehemu ya utekelezaji wa maelezo hayo, tayari TPA imepenga kuongeza vitendea kazi kama Kreni mbili zenye uwezo wa kubeba tani 160 za mzigo kila moja ili kuongeza ufanisi wa huduma katika usafirishaji wa zao la Korosho katika Bandari ya Mtwara.
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho
washiriki wa mkutano huo