Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imeshinda tuzo ya mshindi wa tatu kwa taasisi za umma kwa utoaji huduma bora. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku tatu wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini hivi karibuni. TPA ni miongoni mwa mashirika yaliyoshiriki katika mkutano huo ambapo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan aliikabidhi tuzo hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Dkt. Elinami Minja ambaye aliongozana na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Plasduce Mbossa.