TPA YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 97 YA KILIMO NA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI LUSAKAM, ZAMBIA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imeshiriki katika Maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika kuanzia Julai 30 hadi Agosti 04,2025 katika viwanja vya maonesho ya Biashara Jijini Lusaka, Zambia.
Maonesho hayo yaliyoshirikisha nchi 25 kutoka Barani Afrika, Asia na Ulaya, yamefungwa na Rais wa Jamhuri ya Botswana Mhe. Duma Boko, ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeng’ara ikitwaa Tuzo mbili za nafasi ya pili katika Sekta za Uchukuzi na Afya.
Ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo uliratibiwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Zambia na kushirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH).