Sélectionnez votre langue

Bandari ya Dar es Salaam, terehe 2 Januari 2026 imepokea meli ya kitalii inayoitwa The Crystal Symphony ikiwa na watalii 516 ambao wametembelea vivutio mbalimbali hapa nchini.

‎Wakala wa Meli hiyo Bw. Gilbert Nikata, amesema meli hiyo ya kifahari inaurefu wa mita 238 kina cha mita 8 imefika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea Msumbiji, itakaa kwa siku moja na kuelekea Zanzibar.

‎Pamoja na mambo mengine ameipongeza Serikali kupitia TPA kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari hiyo pamoja na huduma bora bandarini hapo na kuahidi ujio wa meli nyingine zaidi za kitalii.