Sélectionnez votre langue

Bandari ya Dar es Salaam inatarajia kuhudumia tani milioni 32 za shehena ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni matokeo ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika shughuli za uendeshaji na utoaji huduma za kibandari.
Kauli hiyo imetolewa Mei 6, 2026 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abed Gallus Abed, wakati wa hafla ya kampuni ya DP World kukabidhi gari la wagonjwa (ambulance) kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). 

Bw. Abed amesema kuwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika ongezeko la uhudumiaji wa shehena bandarini, suala la usalama na afya limeendelea kupewa kipaumbele maalum. Ameeleza kuwa ujio wa gari hilo la wagonjwa utaimarisha huduma za dharura na kusaidia kulinda usalama pamoja na afya za wafanyakazi na watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam.Akizungumza kwa niaba ya DP World, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Elitunu Malamia, amesema makabidhiano hayo yanaakisi ushirikiano mzuri wa kikazi uliopo kati ya TPA na DP World katika kuendeleza huduma bora na salama bandarini