Sélectionnez votre langue

Bandari ya Mtwara imeendelea kuimarisha nafasi yake kama lango muhimu la biashara ya kikanda baada ya kuhudumia meli 4 ndani ya wiki moja na kushusha zaidi ya magari makubwa 1,500. Magari hayo yanahudumia soko la ndani pamoja na kusafirishwa kwenda nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia (DRC), Zambia na Malawi kupitia Ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor), hatua inayoendelea kuongeza imani ya wafanyabiashara wa ndani na kimataifa katika kutumia bandari hiyo.
Mafanikio haya yametokana na maboresho yanayoendelea kufanywa na TPA, yakiwemo:
Uboreshaji wa miundombinu ya bandari.
Matumizi ya vifaa na teknolojia za kisasa.
Uwekezaji katika mifumo ya TEHAMA.
Punguzo la baadhi ya tozo.
Kuimarishwa kwa utoaji wa huduma kwa viwango vya ubora na weledi.