Sélectionnez votre langue

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wanawake wa Bandari ya Tanga wametoa msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya Tsh 5,419,000 katika kituo cha “Goodwill Children’s Home “kilichopo kata ya Mwahako Wilaya ya Tanga mjini.

Sambamba na kukabidhi msaada huo wanawake hao walijumuika na watoto hao katika futari maalumu iliyoandaliwa na wafanyakazi hao katika viwanja vya Club ya Bandari.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Peter Millanzi, aliwapongeza wanawake hao kwa kufanya matendo ya huruma kwa watoto hao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani jambo ambalo ni baraka na faraja kwa wenye uhitaji.

Awali wanawake hao walishiriki kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo Wilaya ya Tanga mjini maadhimisho hayo yamefanyika tarehe 5 Machi ,2025 na kauli mbiu ya mwaka 2025 ni “ Wanawake, Wasichana 2025 Tuimarishe Haki , Usawa na Uwezeshaji”