Sélectionnez votre langue

 Mwenyekiti wa Bandarini SACCOS Ltd, Bw.Ernest Nyambo ametoa shukrani na pongezi kwa Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ushirikiano inautoa kwa taasisi hiyo ya kifedha.
Bw.Nyambo ametoa shukrani hizo alipotembelea banda la TPA lililopo katika Viwanja vya Nzuguni kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane).
Aidha, Bw.Nyambo ametumia fursa hiyo kuendelea kuwasihi wanachama ambao ni watumishi wa TPA kuendelea kutumia huduma za Bandarini SACCOS Ltd na kuwa Mabalozi kwa watumishi wengine ambao siyo wanachama ili waweze kujiunga na kutumia fursa zilizopo chamani.