Sélectionnez votre langue

Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Joseph Msambichaka, imeridhishwa na viwango vya usalama na ufanisi wa matumizi ya Midaki ya ukaguzi wa makasha katika Bandari ya Dar es Salaam, kufuatia ziara ya kikazi iliyofanyika Julai 28, 2026.
Ziara hiyo ililenga kujionea namna Midaki inavyotumika katika ukaguzi wa makasha pamoja na kufuatilia jinsi TAEC inavyotekeleza jukumu lake la kusimamia matumizi salama ya teknolojia ya mionzi inayotumika katika vifaa hivyo. Akizungumza baada ya kutembelea eneo la ukaguzi, Prof. Msambichaka alisema ameridhishwa na namna shughuli za ukaguzi zinavyotekelezwa kwa kuzingatia viwango vya usalama vinavyowalinda wafanyakazi, madereva na wadau wengine wanaohudumiwa bandarini.