Sélectionnez votre langue

Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) tawi la Makao Makuu wamepongezwa kwa ushindi baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika mwanzoni mwa mwezi Februari, 2026.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Majadiliano (JIC)  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mha. Dkt. Baraka R. Mdima, tarehe 15 Machi 2026 wakati akifungua kikao cha (60) cha Baraza hilo mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

 

Amesema kuwa DOWUTA ni kiungo katika kuimarisha mahusinao kati ya Wafanyakazi na Menejimenti ya TPA na kuwa chachu ya mafanikio katika kazi.

 

“Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Napenda kuipongeza timu mpya ya Uongozi wa DOWUTA ikiongozwa na Falician Hasunga ikiwa ni sehemu muhimu ya mafanikio ya TPA kwa sababu katika kazi zote tunazofanya mahusiano mazuri kati ya Wafanyakazi na Menejimenti ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya kazi.” Amesema Mdima.

 

Aidha amewahakikishia ushirikinao muda wote katika mambo mbalimbali ili kupata mchango wa kila mmoja na pia kuwa timu moja ambayo kupitia majadiliano italetea matokeo chanya katika kuipeperusha bendera ya TPA.

 

Pamoja na Mambo mengine Baraza hilo limempongeza Mwenyekiti wa DOWUTA tawi la Makao Makuu aliyemaliza muda wake Bw. Benjamin Kihanga kwa Uongozi uliotukuka na kuwaandaa vema aliowaachia kijiti na kumuomba kuendelea kutoa usaidizi pale utakapohitajika.

 

Baraza la Majadilioano (JIC ) linafanya kikao cha siku mbili (2), kikilenga kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa yatokanayo na kikao cha 59  na kusaini Makubaliano yaliyofikiwa katika kikao cha (60) cha Baraza Dogo la Majadiliano (JIC) Makao Makuu

.