Sélectionnez votre langue

Baraza Dogo la Majadiliano (JIC) la Bandari za Ziwa Victoria limesisitiza umuhimu wa ushirikiano, bidii na mawasiliano bora miongoni mwa wafanyakazi katika kuongeza tija na ufanisi wa utendaji kazi wa Mamlaka. 
Msisitizo huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bi. Rosemary Ndesamburo, ambaye pia ni Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, wakati wa Kikao cha 62 cha Baraza Dogo la Majadiliano (JIC) kilichofanyika tarehe 16 na 17 Septemba 2026. Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji na maendeleo ya Bandari za Ziwa Victoria, ikiwemo mafanikio yaliyopatikana, pamoja na masuala yanayohusu maslahi na ustawi wa wafanyakazi, kwa lengo la kuimarisha mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka. Akizungumza katika kikao hicho, Bi. Ndesamburo amewasisitiza wajumbe kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano na upendo, huku wakizingatia wajibu wao katika kuhakikisha mijadala na maamuzi ya Baraza yanakuwa na mchango chanya katika kuongeza tija na ufanisi wa utendaji kazi. Amesema JIC linaendelea kuwa jukwaa muhimu la mawasiliano, ushirikiano na uelewano mahali pa kazi, linalowezesha kujadili masuala mbalimbali ya wafanyakazi na taasisi kwa pamoja, hatua inayolenga kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na kufanikisha malengo ya Mamlaka.