Sélectionnez votre langue

Kampuni ya Lojistiki kutoka nchini Rwanda, African Global Logistics (AGL), imefanya ziara ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Bandari Kavu za Ihumwa na Isaka, kwa lengo la kutathmini fursa zilizopo za uwekezaji katika sekta ya uchukuzi na lojistiki nchini.

Katika ziara hiyo, ujumbe wa AGL ulipata fursa ya kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara, ambaye aliukaribisha ujumbe huo na kueleza matarajio ya Serikali kwa kampuni hiyo.

Profesa Kahyarara alisisitiza umuhimu wa mchango wa AGL katika kuongeza tija, ufanisi na ushindani katika Sekta ya Uchukuzi nchini, hususan katika kuimarisha huduma za bandari na usafirishaji wa mizigo.