Sélectionnez votre langue

Meneja wa Bandari ya Tanga Bw.Salehe Mbega, amesema ataendelea  kutatua changamoto za wafanyakazi mara tu zinapojitokeza ili  waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuleta tija.

Bw. Mbega amesema hayo wakati akifungua kikao cha 69 cha Baraza dogo la Majadiliano (JIC) kwa Bandari ya Tanga, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano katika Jengo la Bandari (Bandari House). 

Alisema kuwa changamoto hasa za kimaslahi kwa wafanyakazi ni muhimu kupewa kipaumbele, kwani sizipotatuliwa zinaweza kupunguza ari za wafanyakazi katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha Bw. Mbega alisisitiza zaidi kwa kusema kuwa, hoja za changamoto nyingine sio lazima zisubiri vikao vya baraza ni vyema kuwasilishwa kwake mapema ili zitatuliwe kwa wakati.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyaka wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) Mkoa wa Tanga, Bw.Aliko Mwakipagala, ametoa pongezi kwa Idara ya Usaidizi wa Biashara kwa kutatua changamoto za wateja haraka pindi zinapojitokeza. 

“ Ukweli lazima usemwe idara ya biashara imekua ikitatua changamoto za wateja kwa haraka hasa katika upande wa mifumo inapotokea tatizo wamekuwa msitari wa mbele kuhakikisha tatizo linatatuliwa kwa kweli nawapongeza sana kwa hili “ alisema Bw. Mwakipagala.

Uchaguzi 2025 Logo