KIKAO CHA 74 BARAZA LA WAFANYAKAZI LA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Chama cha Wafanyakazi wa shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) wa Bandari ya Dar es Salaam wapongezwa kwa kudumisha amani iliyopelekea kuimarika kwa utendaji katika Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na wafanyakazi hao wakati akifungua kikao cha 74 cha Baraza la Wafanyakazi la Bandari ya Dar es Salaam mjini Bagamoyo hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed, amewasihi wafanyakazi hao kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
“Mwaka uliopita tumefanya vizuri kwa kuwa na tofauti ya tani Milioni nne (4) tu ya lengo tulilojiwekea, mwaka huu tunatarajiwa kufanya vizuri zaidi, hivyo tuwe tayari kufanya kazi kwa ufanisi na ushirikiano pamoja na waendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ili kutimiza malengo yetu,” amesema Bw. Galus.
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kimelenga kupokea na kujadili utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2024/205 na mpango kazi na Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.