Sélectionnez votre langue

Meneja wa Bandari ya Tanga Bw.Salehe Mbega, amewapongeza Wadau wa Bandari ya Tanga kwa ushirikiano katika utoaji wa huduma bora kwa wateja. 

Bw. Mbega ametoa pongezi hizo wakati wa Kikao cha Kamati ya Maboresho ya Bandari ya Tanga (Port Improvement Committee - PIC) kilichojumuisha wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Katika kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Bandari (Bandari House) Jijini Tanga, Bw. Mbega ambaye hicho ni kikao chake cha kwanza tangu ateuliwa kuwa Meneja wa Bandari ya Tanga, alisema kwa sasa shehena imekuwa ikiongezeka kutokana na ushirikiano mkubwa wa wadau wa bandari.

Bw. Mbega ameongeza kuwa wadau ni kiungo muhimu katika maendeleo na ufanisi wa Bandari ya Tanga, hivyo kama kuna changamoto zinazojitokeza ni muhimu kuzitatua kwa pamoja na kwa haraka ili kuendelea kuwavutia wateja kutumia bandari hiyo.

“Sisi sote tunajenga nyumba moja, ambayo ni Bandari hii ya Tanga, hivyo ikifanya vizuri sifa zinakuja kwetu sote lakini pia tukikosea basi lawama zote pia zitakuja kwetu, hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa ushirikiano,” amesema Bw. Mbega. 

Uchaguzi 2025 Logo