MENJIMENTI YA TPA NA TRC YATEMBELEA BANDARI KAVU YA KWALA IKIWA NI UKAGUZI WAMAADALIZI YA UZINDUZI NA MHE. RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) IJP Mstaafu Balozi Ernest Mangu akiwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC) Mha. Machibya Shiwa na Viongozi wengine, Julai 25,2025, wametembelea Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Vigwaza, Kibaha Mkoa wa Pwani, kukagua maandalizi ya uzinduzi wake na usafirishaji wa Shehena kwa treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma, unaotarajiwa kufanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wake Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Julai 31,2025.