Sélectionnez votre langue

Jumla ya Wafanyakazi 50 wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), wakiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu, Bw. Freddy Liundi, tarehe 30 Machi, 2026 wametembelea Bandari Kavu ya Kwala ili kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali za utekelezaji Bandarini hapo.

 

Ziara hiyo, imelenga haswa kujifunza kuhusu mifumo ya uendeshaji wa bandari, taratibu za usafirishaji wa mizigo, pamoja na fursa zilizopo katika kuboresha biashara ya kimataifa kupitia bandari hiyo.

Bandari hiyo Kavu iliyopo Vigwaza, Kibaha, Mkoa wa Pwani ina hekta 502 (hekta 120 zimesafishwa, ambapo 60 kati ya hizo zimesawazishwa na kujengwa uzio wenye urefu wa Km 2.96, huku hekta 5 zikijengwa kwa  sakafu ngumu kwa kiwango cha zege).

 

Kwa sasa Bandari Kavu ya Kwala ambayo inapokea treni 1 hadi 2 kwa siku ikiwa na makasha ya mizigo huku uwezo wake ikiwa ni kuhifadhi makasha 3,500 kwa wakati mmoja, itasadia kupunguza msongamano wa bandari ya Dar es Salaam kwa 30%.

 

Bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku sawa na makasha 300,000 kwa mwaka