MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TASAC ATEMBELEA BANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha. Mussa Mandia ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kufanya maboresho katika miundombinu ya kuhudumia shehena katika Bandari zote nchini.
Nahodha. Mandia ametoa kauli hiyo Julai 05,2025 alipotembelea banda la TPA katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.