Sélectionnez votre langue

Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imewakutanisha Wadau wa Bandari Kavu katika kikao kilicholenga kujadili changamoto,kupokea mawazo na kubadilisha panapohitajika ili kuongeza ufanisi katika uhudumiaji wa shehena.

 

Kikao hicho kilichofanyika Aprili 16, 2026 Makao Makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam, kiliongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano

Dkt.George Fasha ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi alisema TPA inatambua umuhimu wa Bandari Kavu katika ufanisi wa shughuli za kibandari nchini.

 

Aidha Dkt. Fasha aliwataka washiriki wa kikao hicho kujadili kwa uwazi kuhusu maeneo yanayohitaji maboresho na  ufanisi katika kuhamisha, kuhifadhi na kushughulikia shehena ndani na nje ya eneo la Bandari Kuu.

 

Akizungumza kikaoni hapo,Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bandari Kavu Nchini (CIDAT) Bw.Melickzed Kishange alisema vikao aina hii vina umuhimu mkubwa kwa wadau Bandari Kavu kwani ndio jukwaa litalohadili na kutatua changamoto zitokanazo na shughuli za uhamishaji wa shehena kutoka bandarini.