Sélectionnez votre langue

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA.Dkt.Habibu J.Suluo, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa utendaji wenye matokeo chanya. CPA.Dkt. Suluo amesema hayo Agosti 5,2026 mara baada ya kutembelea banda la TPA katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Amesema nchi inajivunia utendaji wa TPA na fursa za kibiashara zinatokana na utendaji huo uliotukuka.