VIONGOZI WAIPONGEZA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA
Viongozi mbalimbali wameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ufanisi katika kuhudumia shehena na uboreshaji wa miundombinu ya kibandari pamoja na ushirikishwaji wa sekta binafsi.Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la TPA katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma,Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Regina Ndege Qwaray ( Mb) ameipongeza TPA kwa ufanisi katika uhudumiaji shehena na kudhibiti mianya ya upotevu wa mizigo ya wateja.Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Selemani Mkomi ametoa pongeza kwa Menejimenti ya TPA kwa ufanisi wa Bandari zote Nchini. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara amepongeza ufanisi katika uhudumiaji wa meli kwa uharaka.Naye Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA. Dkt. Habibu J.Suluo ametoa pongezi kwa Bodi,Menejimenti na watumishi wote wa TPA kwa kazi nzuri ya kuifanya Tanzania kuwa lango kuu la biashara ya Kitaifa na Kimataifa na kwamba historia itawakumbuka.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"