Sélectionnez votre langue

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepongezwa kwa kukutanisha Wadau wa Bandari ya Mtwara kwa lengo kujadili ili kuiwezesha bandari hiyo kuendelea kuhudumia zao la korosho kuelekea masoko ya kimataifa. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Bandari ya Mtwara uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), mjini Mtwara.  Aidha Mhe. Mwaipaya amesema Serikali ya awamu ya sita chini Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeijengea Bandari ya Mtwara uwezo kwa kuimarisha miundombinu ya kuhudumia 
shehena ili kuongeza ufanisi zaidi. Awali katika salamu za ukaribisho,Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha.  Dkt. Baraka Mdima kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, amesema lengo la Mkutano huo ni kujadiliana kwa uwazi  changamoto,mafanikio na namna bora ya kutafuta ufumbuzi utakaoongeza ufanisi wa uhudumiaji wa shehena. Naye Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi ameeleza ufanisi na utayari wa Bandari hiyo katika msimu mpya wa korosho kwa kuongeza vifaa vya kuhudumia meli kama Gottwald na Folklift.