Sélectionnez votre langue

Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega amewapongeza wafanyakazi wa Bandari hiyo kwa kuchapa kazi kwa bidii na kuiwezesha kupata mafanikio makubwa.

Bw. Mbega ametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha 39 cha Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Tanga kilichofanyika bandarini hapo.

Katika kikao hicho, Baraza lilipokea taarifa ya utendaji kazi wa Bandari ya Tanga kwa kipindi cha miezi sita ya Julai hadi Disemba 2025. Pia Baraza hilo lilijadili mapendekezo ya malengo na bajeti mpya ya Bandari kwa mwaka wa fedha 2026/ 2027.

Aidha Baraza hilo lilikubaliana kuendelea kufanya kazi ufanisi mkubwa ili kupata tija kubwa zaidi katika kuhudumia wateja wanaopitishia mizigo yao katika Bandari ya Tanga.

Aidha katika hatua nyingine, Bw. Mbega amewashukuru wajumbe wa baraza hilo kwa mchango wao ulioiwezesha Bandari ya Tanga kupata mafanikio makubwa.