Sélectionnez votre langue

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wamepongezwa kwa kuitangaza TPA kupitia michezo kitaifa na kimataifa.Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Dkt. Baraka R. Mdima kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce M. Mbossa wakati wa kikao cha kawaida cha (59) cha Baraza la Majadiliano (CJIC) kinahofanyika mjini Morogoro.Amesema kuwa Menejimenti inatambua mchango wa Wafanyakazi katika Kuitangaza 
TPA katika michezo mbalimbali ikiwemo Kandanda, Mpira wa Wavu, Mpira wa pete, pamoja na Kwaya na kusisiza juhudi hizo kuwa endelevu.Mha. Dkt. Mdima amasema kuwa katika kukuza na kuendeleza juhudi hizo, Mkurugenzi 
Mkuu ameunda Kamati maalum itayokayosimamia shughuli zote za michezo ili kuiendeleza na kuitangaza TPA kitaifa na kimataifa pamoja na kulinda taswira ya Taasisi.Baraza la Wafanyakazi (CJIC) linakutana kwa siku mbili, likiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Claudio Mbena. Pamoja na mambo mengine Baraza hilo liliwaaga Wastaafu waliomaliza utumishi wao kisheria ambao kwa upande wa Wajumbe wa DOWUTA ni Bw.Telela Telela, Bi. Celina Simon, Bw. Benjamin Kihanga, Bw. Juma Bin Juma, Bw. Ernest Kijika na Mjumbe upande wa Menejimenti ni Meneja Bandari ya Mwanza Bw. Manga