Sélectionnez votre langue

Wajumbe wapya wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) tawi la Dar es Salaam wameaswa kutumia fursa waliyoipata kwa kufanya kazi kwa weledi ili matarajio ya wanaowawakilisha kuweza kufikiwa kwa ufanisi.

 

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed wakati akifungua Baraza la Majadiliano (JIC) la Bandari ya Dar es Salaam linalofanyika mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

 

Amesema kuwa dhamana waliyoipata wanategemewa kwa kiasi kikubwa na Wafanyakazi na pia kama  watunga sera  au wapitishaji wa mikakati wa mambo yote ya Bandari,  hawana budi  kujitoa na kufanya kazi kwa uaminifu wa hali ya juu ili matarajio ya wale wanaowawakilisha yaweze kufikiwa.

 

Aidha Bw. Abed amewapongeza wajumbe hao wa Baraza kwa kuchaguiwa kuwa wawakilishi wa Wafanyakazi na kuwasihi kuwa tayari kujifunza kwa waliowatangulia na kutumia nafasi waliyoipata kuendeleza Taasisi ya TPA.

 

Pamoja na mambo mengine Baraza hilo limefanya uchaguzi mdogo na kuteua makatibu wapya badala ya Walioshika nyadhifa hizo kujiuzuru ambapo Katibu amechaguliwa Bi.Moni Msemo na Katibu Msaidizi ni Bw. Nasibu F. Wallase.

 

Waliojiuzuru ni pamoja na aliyekuwa Katibu Bw.Agripa Mjema na katibu Msaidizi Bw. Egidius K. Glegory wote kwa sababu za kiutumishi.

 

Baraza la Majadiliano (JIC) la Kituo cha Bandari ya Dar es Salaam limelenga kujadili maslahi ya Watumishi na maboresho ya mazingira ya kazi kwa leng kuongeza ufanisi