Sélectionnez votre langue

Maafisa wanafunzi na Wakufunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kikosi Maalum kilichopo Sangasanga Wilaya ya  Morogoro leo tarehe 3 februari 2026 wametembelea Bandari ya Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejifunza shughuli za Bandari pamoja na namna TPA ilivyojidhatiti na utayari wake katika kupambana na hatari za kiusalama katika Bandari zake hususan Bandari ya Dar es Salaam ambalo ni langu kuu la Biashara kitaifa na kimataifa.

Ziara hiyo imeongozwa na Meneja Ulinzi na Usalama Bw. Said J. Mollel Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed.