Sélectionnez votre langue

Bandari ya Tanga imetoa rai kwa Watumishi wapya walioripoti kituoni hapo kufanyakazi kwa bidii na kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma ili kuhakikisha wanatoa huduma bora yenye tija wakati wote.

 

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Peter Millanzi alipokuwa akiongea na watumishi hao alipokuwa anawakaribisha rasmi.

 

Bw. Millanzi aliwapongeza watumishi hao na kuwataka kutumia vizuri  taaluma waliyonayo katika kutimiza vyema majukumu yao kwa weledi na ufanisi sambamba na kutii sheria na kanuni za utumishi wa umma.

 

“Kazi za bandari zinatuunganisha na wateja, na ni wajibu wetu kuhakikisha tunawahudumia kwa ukarimu na upendo huku tukifuata miongozo iliyowekwa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma”. Aliongeza Bw. Millanzi.

 

Awali akitoa salamu kwa Watumishi hao Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari  (DOWUTA) tawi la Tanga, Bw. Aliko Mwakipagala aliwapongeza watumishi hao na kuwasihi kutojihusisha na tabia zozote zitakazoiletea taasisi taswira mbaya  kama vile rushwa, udokozi, utoro na kuchelewa kazini, ulevi na uzembe eneo la kazi.

 

Bandari ya Tanga imepokea watumishi wapya 33 wenye taaluma nyanja mbalimbali ikiwa ni mpango mkakati wa serikali katika kutimizia ahadi zake kwa watanzania katika utoaji wa ajira nchini