WAZEE MAZINGIRA MAGUMU WAGUSWA NA WANAWAKE BANDARI YA MTWARA
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake wa Bandari ya Mtwara umeonesha moyo wa kujali jamii kwa kutoa msaada wa magodoro 13 yenye thamani ya shilingi 2,210,000/= pamoja na mifuko 10 ya sabuni kwa ajili ya kuwasaidia wazee wanaoishi katika mazingira magumu.
Msaada huo umekabidhiwa tarehe 6 Machi, 2026 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake ngazi ya Wilaya yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Naliendele. Hatua hiyo imelenga kuonesha mshikamano na kuwajali wazee wanaohitaji msaada katika jamii.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Abdallah Mwaipaya ambapo katika hotuba yake aliwahimiza wanawake wa Mtwara kuendelea kuwa na umoja, bidii na uthubutu katika shughuli zao za maendeleo.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"