ZIARA YA MRADI WA UBORESHAJI WA BANDARI YA KIGOMA JULAI 20,2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Julai 20,2026 anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa meli nne za mizigo na ziara ya miradi ya uboreshaji wa Bandari ya Kigoma. Akizungumza na Waandishi wa habari Julai 19,2026, mkoani Kigoma, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), amesema Mkoa wa Kigoma unaunganishwa na Ziwa Tanganyika ambalo ni lango muhimu la usafirishaji na biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia. Aidha Mhe.Prof.Mbarawa amesema utekelezaji wa miradi hii utawezesha Mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuhudumia masoko makubwa ya nchi hizo na kuimarisha Ushoroba wa Kati.
Pia, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa alikagua moja kati ya Meli 4 za mizigo zitakazozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Julai 20,2026 katika Bandari ya Kigoma pamoja na miradi ya maboresho katika Bandari ya Kigoma, ikihusisha maboresho ya gati la kuhudumia Shehena ya mizigo, gati la kuhudumia Abiria, Jengo jipya la Abiria na barabara ya kuingia na kutoka Bandarini, inayojengwa kwa kiwango cha zege ikiwa na urefu wa mita 481.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"