Meli kubwa ya Makasha ya Mv Nordic Bc Munich imetia nanga katika gati jipya la Bandri ya Tanga. Hii ni mara ya kwanza kwa meli yenye urefu wa mita 180 na kina cha mita 7.4 kutoka nchini India kutia nanga katika bandari hiyo. Ujio wa meli kubwa kama hizi, ni matokeo ya maboresho ya mradi mkubwa wa Bandari ya Tanga, kwa sasa Bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia meli kubwa gatini, amesema Meneja Bandari ya Tanga, Mrisha Mrisha. Meli hiyo imebeba shehena ya mabomba kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji katika Mkoa Tanga. Mradi huo una lengo la kutoa maji kutoka Mto Pangani kwenda katika miji ya Pangani, Muheza, Korogwe na Handeni. Mwisho