Bandari ya Mtwara na nyingine za Bahari ya kusini

Bandari ya Mtwara ni miongoni mwa bandari kuu tatu zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliyopo Kusini mwa Tanzania karibu na mpaka na Msumbiji.

Kijiografia inapatikana kilomita 578 Kusini mwa Jiji la Dar es Salaam. Bandari ya Mtwara ambayo ina kina kirefu ilijengwa kati ya mwaka 1948 na 1954. Ujenzi wa awali na uendelezaji wa bandari hiyo uliendana na ujenzi wa reli kuanzia Mtwara hadi Nachingwea.

Sifa za Bandari

Eneo la gati lina kina kirefu cha meta 9.5 hadi 13.5, hakuna masharti ya maji kupwa na maji kujaa kwa meli zinazoingia na kutoka bandarini.

Nyenzo za Bandari

Ukuta wa Gati

Bandari ina ukuta wa gati wenye urefu wa mita 385 unaoweza kutia nanga meli mbili na chombo kimoja cha mwambao kwa wakati mmoja. Kina cha meli ni mita 9.85 nakutokana na vifaa vya sasa vya kuongozea meli vinavyotumia umeme wa jua, meli zitaingia muda wote (saa 24)

Miundombinu ya Bandari

Bandari ina gati lenye urefu wa meta 385 linalowezesha meli nne kutia nanga na chombo kimoja cha mwambao kwa wakati mmoja. Bandari hii ikiwa na kina cha meta 9.5 hadi 13.5 huku ikiwa na vifaa vya kisasa vya kuongozea meli vinavyotumia umeme wa jua, meli zinaweza kuingia bandarini muda wowote katika saa 24 za siku.

Vifaa

Miundombinu ya kuhudumia shehena iliyopo ni pamoja na zana mbalimbali za kupakilia, kupakulia na kupanga. Zana hizo ni kreni kubwa ya kupakia na kupakua shehena za makasha kwenye meli (SSG), winchi inayotembea yenye uwezo wa tani 100, Reach Stacker zenye uwezo wa kubeba tani 45 kila moja, Front Loader tani 42, winchi zinazotembea zenye uwezo wa tani 50 na tani 25, mitambo ya kubeba makasha matupu,foko zinazobeba tani 16, tani 5 na tani 3 , matrekta, Hoppers na Grabs.

Kuna mashua za kusogezea meli na kuongoza (Tug Boat na Mooring Boat). Bandari ya Mtwara ina vifaa vingi na imejiandaa kuhudumia aina zote za shehena kwa saa 24 siku saba kwa wiki. Pamoja na bandari ya Mtwara zipo bandari ndogo za Lindi na Kilwa.

Maghala

Kuna ghala kuu mbili za shehena zenye jumla ya zaidi ya eneo la mraba 15,000. Hifadhi ya wazi iliyojengwa kwa jumla ya meta za mraba 124,000 ikijumuisha meta za mraba 76,000 iliyojengwa mwaka wa 2020. Hifadhi ya wazi ya meta za mraba 20,000.

Uwezo wa Sasa

Bandari ya Mtwara inaweza kuhudumia tani 1,000,000 za shehena zinazoingizwa na kusafirishwa nje kwa mwaka. Bandari hii imejengwa hasa kuhudumia bidhaa mchanganyiko na makasha.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-

Meneja wa Bandari Mtwara,
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
S.L.P 530,
MTWARA, Tanzania

Simu. +255 (23) 2333125
Faksi +255 (23) 2333153
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.