Huduma Shirikishi

01

Polisi na Zimamoto

Bandari siku zote inatakiwa kuwa katika hali ya kuwezesha shughuli zake kwenda kwa usalama. Kutokana na mazingira hayo kunatakiwa kuwepo na vyombo vya usalama na pia vya kuhudumia afya za wafanyakazi. Huduma zilizopo ni za polisi na zimamoto bandarini ambazo zinapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki. Kikosi cha zimamoto kina vifaa vya kutosha kuweza kukabiliana na dharura yoyote ile ndani ya bandari na jirani.

Kikosi hiki kikijumuisha wataalamu wa uokoaji wenye uzoefu, wakiwa na vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu kipo tayari kukabiliana na chochote kinachotokana na milipuko ya moto au hatari za kemikali na kibayolojia.Kikosi hiki hufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuhakikisha wafanyakazi, wageni na watumiaji wengine wa bandari wamejiandaa vyema kwa dharura yoyote ile. Mazoezi hayo hutumika kupima muda na uwezo wa kukabiliana na hali hiyo na kutumika zaidi kuwafunza wahudumu wa dharura, wafanyakazi na watumiaji wa bandari ili kudumisha hali ya utayari. Kikosi hiki pia kinashiriki katika juhudi za kuzima moto nje ya maeneo ya bandari kwa kushirikiana na mamlaka husika.

02

Matibabu na Gari la Wagonjwa

Timu ya matibabu ya TPA imejipanga kukabiliana na dharura ndani na maeneo ya karibu na bandari. Timu zinafanya kazi na Afisa Mkuu wa matibabu kuhakikisha kuwa wafanyakazi na watumiaji wengine wa bandari wako katika hali nzuri ya kiakili na kimwili.

Kuna vituo maalumu vya afya vyenye vifaa vya kisasa na wataalamu wenye uwezo wa kutoa huduma na kuokoa maisha. Pia kuna huduma ya ambulansi ya saa 24. Pia kuna kituo cha mazoezi ya viungo chenye vifaa kamili vya mazoezi ya mwili na wataalamu ili kuwaweka katika hali njema kisaikolojia na kimwili wafanyakazi na kuzuia magonjwa nyemelezi.