Usalama na Ulinzi

Ili kuimarisha masuala ya afya na usalama ndani ya eneo la bandari, watumiaji wa bandari wanahitajika kuwa na nidhamu ya hali ya juu.
Ifuatayo ni miongozo inayostahili kufuatwa kwa lengo lakuhakikisha kuna usalama

Safety Ribbon TPA sw

Alama za Usalama

Kila mfanyakazi ni lazima afuate alama za usalama zilizowekwa kwenye maeneo mbalimbali bandarini. Kwa mfano alama ya utelezi, kipito cha reli na kadhalika Kutofuata alama hizi kutasababisha ajali na ikigundulika umekiuka sheria za usalama za TPA, hatua kali za nidhamu zitachukuliwa dhidi yako.

Uendeshaji magari

Undeshaji magari na vyombo vya moto katika bandari mwendokasi wake usidizidi kilometa 20 kwa saa. Mtumiaji wa bandari anatakiwa kufuata Sera ya Usalama na Afya ya TPA, ili kuboresha usalama na Afya. Katika eneo la Bandari kuna mitambo mikubwa ambayo daima ipo kazini, kwa hiyo mwendo kasi unaweza kusababisha ajali.

Kuegesha

Hutakiwi kuegesha chombo cha moto kwenye njia ya reli kwani unaweza kuhatarisha maisha na mali za wateja. Hauruhusiwi kwa namna yoyote ile kuziba barabara yoyote ndani ya eneo la Bandari ambalo linahitajika kutumika kwa magari mengine na ya zimamoto kuweza kupita kwa urahisi na haraka wakati wa dharula.

Mavazi ya Usalama

Wafanyakazi wote watakaokuwa wanaohudumia shehena ni lazima waelewe kwa ukamilifu au kupata mafunzo ya jinsi ya kujilinda na kujikinga dhidi ya ajali na matukio mbalimbali hatarishi.
Tumia mavazi halisi ya usalama nyakati zote unapokuwa kazini kwenye shughuli za Bandari. Mavazi haya ya usalama ni kama vile fulana zinazo akisi mwanga, mabuti, viatu vya usalama, kofia ngumu na mengineyo.
Kwa hiyo kila mfanyakazi ni lazima avae vifaa vya kinga binafsi (PPE) wakati wote wanapokuwa eneo la bandari. Kushindwa kufanya hivyo itakuwa kinyume na sheria za usalama za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na kusababisha adhabu kwa kutofuata sheria hizo.

Kizima Moto

Tumia vifaa sahihi vya kuzimia moto na hakikisha moto umezimika. Vifaa vya kuzimia moto vipo kila mahali pa kujazia mafuta kwa urahisi na uharaka wa kukabili moto mahali hapo. Aina ya vifaa vya kuzimia moto ni lazima viwe kemikali kavu ya Unga (Dry Chemical Powder) au Kaboni Dioksaidi (Carbon Dioxide) au Povu (Foam).

Idara ya tahadhari ya majanga ya moto, afya na mazingira itawapanga wazima moto kuwa tayari wakati wote wa utendaji kazi.

Mawasiliano

Iwapo utaona moto mahali popote eneo la bandari jaribu kuuzima kwa kutumia vifaa vya kuzimia moto vilivyopo na iwapo moto utaongezeka, usiendelee kuuzima kwa kutumia kifaa cha kuzimia moto ulichonacho bali piga simu kituoni kwa Na. 2116287 au 0755195896 au wasiliana na msimamizi wako wa kazi au mlinzi aliye karibu nawe. Kwa kutumia Radio Call yako toa taarifa ya ajali au tukio lolote hatarishi haraka kwenye chumba cha kudhibiti moto au piga kelele za moto ili kuwezesha wengine kuelewa na kuondoka haraka katika eneo la tukio.

Kujaza Mafuta na Kuwasha Gari

Kusudio la kutaka kujaza gari mafuta ni lazima litolewe taarifa kwa Meneja wa Bandari na idara ya Tahadhari ya Majanga ya Moto, Afya na Mazingira. Unapofanya miadi ya siku ya kujaza mafuta kiasi cha mafuta kinachotajwa kutumika ni lazima kioneshwe kwenye barua ya maombi kwa idara ya Moto Bandarini, Afya na Mazingira. Zingatia kuwa shughuli za kujaza mafuta ni lazima zifanywe mahali pa wazi au eneo la kukwepa moto na vifaa vya kujaza mafuta vinavyofaa kama (nozeli za kujazia mafuta) vitumike, hakikisha kuwa hakuna umwagikaji wa mafuta wakati wa kujaza mafuta kwenye gari.

Iwapo eneo limemwagika mafuta ni lazima lisafishe na iwapo hukulisafisha sheria za usalama za TPA zitatumika kukuadhibu. Hakikisha kuwa vyombo vya kuchukulia mafuta kutoka kwenye gari la mafuta kwenda kwenye magari ni vile sahihi kwa aina ya mafuta kama petroli au dizeli.

Kujaza mafuta kwa kutumia vyombo vilevile kwa petroli na dizeli au kinyume chake havitaruhusiwa kwa sababu itasababisha hitilafu kwa injini. Kujaza mafuta kwa utaratibu huo ni kinyume na kanuni za usalama za TPA zitakazo sababisha adhabu na faini kwa uharibifu wa gari.

Wakati wa kujaza mafuta injini ya gari ni lazima izimwe, simu za mkononi zizimwe na uvutaji sigara ni marufuku, tenganisha magari yote yanayobeba vyombo vya mafuta na magari mengine. Tenganisha vyombo vya kubebea mafuta na cheche za moto (kama betri), unapoendesha gari na kubaini kuwa gari lako limepata hitilafu na linashika moto tafadhali usiingie kwenye maegesho yeyote ya magari au kujichanganya na wengine kuepuka kueneza moto.